Mwakilishi wa Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma, Coletha Kilawe akizungumza wakati wa hafla ya Iftar maalumu ya kuliombea dua/sala jengo jipya la Wakala wa Vipimo 9WMA) eneo la Medeli jijini Dodoma Machi 28, 2025.
Akizungumza katika hafla hiyo, Kilawe ambaye ni Afisa Rasilimali Watu wa mkoa huo, amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa serikali anayoiongoza kutoa fedha za ujenzi wa jengo hilo la kisasa uliogharimu zaidi ya sh. bil. 6, lakini pia hakusita kuupongeza uongozi wa WMA kwa kuandaa tukio hilo jema la kuandaa hafla ya iftar maalumu ya kuliombea dua jengo hilo.
Hafla hiyo ilihudhuriwa na baadhi ya viongozi wa dini, siasa, viongozi na watumishi wa WMA pamoja na majirani.
Baadhi ya waalikwa wakijipatia mlo huo.
Mjumbe wa Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Vipimo (WMA), CPA. Swalehe Chondoma akizungumza kwa niaba ya Mwenyekiti wa bodi hiyo.
John Maliga wa EAGT Baraza la CPCT.Askofu Anthony Nyashimba wa Kanisa la Baptist na Mwenyekiti wa Umoaja wa Makanisa ya Kikristo Mkoa wa Dodoma akizungumza wakati wa sala ya kuliombea jengo jipya la WMA.
Sheikh Ahmad Said Msemaji wa Sheikh wa Mkoa wa Dodoma akizungumza wakati wa kuomba dua.
Mkurugenzi wa Biashara wa WMA, Karim Mkorehe akizungumza kabla ya kumkaribisha CPA. Chondoma.
IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA
MSIMAMIZI MKUU
KAMANDA WA MATUKIO ONLINE TV
0754264203
Comments