JWTZ LASAIDIA HUDUMA TIBA NA AFYA JAMHURI YA AFRIKA YA KATI


Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania limechangia huduma tiba na afya  kwenye hospitali ya Jiji la Berberati iliyoko nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati tarehe 14 Aprili mwaka 2025.

Akizungumza mara baada ya uchangiaji wa huduma hizo  kwa niaba ya Kamanda Kikosi cha Nane cha Ulinzi wa Amani nchini humo Luteni Kanali Theophil Nguruwe, Mkuu wa Operesheni na Utendaji Kivita wa Kikosi hicho Maj Mkangara Mzuma amesema kuwa JWTZ limefanya hivyo ikiwa ni moja ya kuimarisha amani nchini humo.

" Siku zote JWTZ linathamini maisha ya watu na linawajibika na kuhakikisha wananchi wanaishi kwa amani na utulivu"alisema Maj Mzuma.

Naye Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo, Daktari Sanzema Komoto amelishukuru JWTZ na uongozi wa Kikosi Cha Nane Cha Ulinzi wa Amani nchini humo kwa moyo wao wa kujitolea ili kurudisha amani kwa wananchi wake.

"Tangu JWTZ lianze ulinzi wa amani nchini kwetu, limekuwa msaada mkubwa kwenye kusaidia huduma za afya na wananchi wetu wamefaidika sana" alisema Daktari Komoto.

Huduma tiba na afya zilizotolewa ni uchangiaji wa damu salama, vyandarua, vyakula, sabuni, maji safi na salama pamoja na usafi wa mazingira ya hospitali hiyo.






 

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

BREAKING NEWS | MKURUGENZI MTENDAJI WA TANESCO AFARIKI DUNIA

SHEREHE ZA DKT. CHANDE KUSIMIKWA UASKOFU MKUU KANISA LA KARMELI ZAFANA

#MAKINIKIA: HEKAYA FUPI YA MJI WA KIHISTORIA WA MOSHI MKOANI KILIMANJARO

HUU NDIO UKWELI ULIVYO RAFIKI YANGU

RATIBA KAMILI YA HARUSI YA DIAMOND, ZUCHU

ZIJUE TABIA 9 ZA WANAWAKE HAWA....

TANZANIA NI MIONGONI MWA NCHI 10 ZINAZOONGOZA KWA MAZAO YA KILIMO AFRIKA

ASKOFU CHANDE ATOA MSAADA WA MAZIWA, AWAOMBEA WATOTO NJITI