Kutoka: Diaspora CCM Southeast U.K.
Wapendwa WanaDiaspora,
Tunawasalimu kwa moyo wa mshikamano na uzalendo. Katika kila ushindani, wapo wanaopenya na wapo wanaobaki – si kwa sababu hawajatosha, bali kwa sababu wakati mwingine nafasi ni chache kuliko uwezo na vipaji vilivyopo.
Kwa wale miongoni mwetu ambao safari ya kuteuliwa haikutimia wakati huu, tunasema hongereni sana kwa ushujaa wenu, moyo wenu wa kujitolea, na uzalendo mliouonesha. Mmekuwa alama ya ujasiri, mkiwakilisha vyema dhamira ya kweli ya WanaDiaspora katika maendeleo ya Chama na Taifa letu.
Kukosa nafasi si kushindwa.
Ni kuahirishwa kwa wakati – lakini si mwisho wa ndoto. Tunaamini fursa zaidi zipo mbele, na mchango wenu bado ni wa thamani kubwa kwa jamii, kwa chama, na kwa Taifa kwa ujumla.
Tunaendelea kuwa wamoja.
Tunaendelea kushikamana.
Na tunaendelea kupigania maendeleo ya kweli kwa Watanzania wote – ndani na nje ya mipaka ya nchi.
Kwa moyo huo huo wa kizalendo, tutaendelea kujenga CCM imara, ya kisasa na jumuishi kwa vizazi vijavyo.
Tuko pamoja – Mbele kwa Mbele.
Kwa niaba ya WanaDiaspora wote,
Diaspora CCM Southeast United Kingdom
Comments