MGOMBEA Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi CCM Rais Dkt Samia Suluhu Hassan amelikubali kulifanyia Kazi ombi kuanzisha bandari ya mifugo katika ufukwe wa Bahari ya Hindi Wilayani Pangani, mkoani Tanga.
Ombi Hilo lilitolewa kwa niaba ya wananchi na Mgombea ubunge wa jimbo la Pangani, Jumaa Awesu wakati wa mkutano wa Kampeni za CCM Pangani Mjini Septemba 29, 2025.
Aidha, Dkt. Samia amelikubali pia ombi lingine la Awesu la kununua boti kwa ajili ya kusafirisha abiria wilayani humo na miji mingine.
Comments