Anaandika, Anold Abel Fanuel.
Ukishakuwa Mkubwa kuna mipira minne( 4 balls) unapaswa uilinde na ujue kuitumia.
1. Ubongo wako.
Huu ni mpira namba moja ambao lazima uulinde na ujue kuutumia.
- Ubongo ndio unaoendesha maisha yako. Huu ndio utaamua uishi maisha ya aina gani. Maamuzi yote ya maisha yako yanatoka kwenye Ubongo.
- Chakula cha ubongo ni Maarifa, ujuzi, elimu, ufahamu.
Kama ilivyo kwa tumbo. Ubongo unahitaji chakula kila siku.
- lazima uwe na tabia ya kujifunza kila siku inayoenda kwa Mungu.
- Kujifunza kuna njia nyingi; Kuna Kusoma; Kama kusoma Makala za kuelimisha kama zangu, kusoma vitabu, Kusoma majarida,
Kuna Kujifunza kwa kwenda shule au kozi.
Kuna kujifunza kwa kutembea na kusafiri.
Kuna kujifunza kwa kuangalia filamu na documentary.
Lazima ujifunze Kijana mwezangu.
- Ubongo ulinde kwa Kula vyakula vyenye afya njema. Lishe bora. Usinywe ukalewa sana. Kunywa maji mengi.
Fanya mazoezi. Pumzika angalau masaa nane. Hiyo ndio njia ya kulinda ubongo wako.
Pia usifikirie mambo ya hovyo. Wala kusoma au kusikiliza vitu vya hovyo. Vinaharibu ubongo na kuzalisha negative energy katika maisha yako.
- elewa: Ubongo ni kama Sumaku, inavuta energy kwenye mazingira unayoishi. Ubongo ukiwa na negative energy unavuta mikosi, mabalaa, na watu wabaya katika maisha yako.
Ubongo wako ukiwa na positive energy, utavuta kwenye mazingira nguvu chanya, bahati, fursa, watu wazuri na utakuwa na maisha yenye furaha.
- Ukitaka Mahusiano mazuri, labda inatafuta mwenza wa maisha. Unapaswa uanze na ubongo wako. Ujaze positive energy kisha utashangaa anakuja mume au mke mwema. Hiyo ni moja ya siri nilizokuambia Mwanangu. Na hivyo ndivyo Babaako nilivyoishi.
2. MOYO WAKO
Moyo wako ni Mpira wa pili nyeti na muhimu ambao unatakiwa uulinde na ujue kuutumia.
- Moyo ndiko ziliko chemchem za upendo na hisia.
- Mwanangu, Hakuna maisha ya furaha bila upendo.
- nilikufundisha kuudhibiti Moyo wako. Nilikuambia moyo uliodhibitiwa hutoa upendo uliodhibitiwa. Upendo uliodhibitiwa huleta furaha
- Dhibiti Moyo wako ili Usiendeshwe na mihemko au hisia
- Nilikuambia Maisha yanaongozwa na kuendeshwa na Ubongo(Akili). Hivyo lazima ujifunze kuutawala moyo wako kama sisi Baba zako Watibeli.
- Moyo kazi yake ni kusukuma Uhai. Kusukuma damu.
- Kusukuma uhai maana yake ni kuwa na msisimko wa maisha, kuwa na hamasa ya maisha, kuwa Motivated. Kuwa na Msukumo katika maisha, shauku na Ari
- Huwezi kufanikiwa katika maisha kama huna msukumo wa ndani. Ndani ya Moyo.
- Ubongo utakupatia ujuzi, elimu, utambuzi, maarifa na ubunifu ambao utautumia kufanya msukumo uliomo ndani kutimiza ndoto na nia yako.
3. Korodani, kende na uume
Huu ni mpira wa tatu.
- Lazima uulinde kwa nguvu zote, ujue na matumizi yake.
- Lazima ujue kudhibiti Uume wako kama nilivyokufundisha
- Sio kila shimo utakaloliona unatakiwa kuingiza Msumari wako. Mashimo mengi ni machafu na yametegwa mitego ya kukuangamiza maisha yako
- sio kila Ukisimamisha au ukiwa na hamu unapaswa kutafuta Mwanamke. Hapana!
Jifunze kujizuia
- Kama itakushinda sana. Tafuta mwanamke mzuri mmoja mwenye sifa kama wanawake wa Tibeli.
Ambazo ni Mwanamke mzuri sana.
Mwanamke Msafi. Sio aliyeingiliwa na wanaume wengi(mchafu)
Mwanamke mbichi. Lazima awe mdogo mdogo kiumri kuliko wewe. Sio uchukue mzee au mkubwa kuliko wewe.
Mwanamke mchapakazi mwenye uwezo wa kuzalisha mali. Wanawake wasio wachapakazi na wasioweza kuzalisha mali hao waachie jamii zingine za watu. Hao sio hadhi yako, sio daraja lako, hamfanani.
- Mwanamke atakayeweza kuitwa Mkeo, mama wa watoto wako lazima awe na sifa za wanawake wa Tibeli.
- Mpira huu unahusu sio tuu starehe na utambulisho wako kama mwanaume bali pia unahusu kiwanda na hatma ya kizazi utakacholeta Duniani.
- Hivyo lazima uwe Mwangalifu
4. MACHO YAKO.
- Mwanaume ana macho manne kama ilivyo kwa mwanamke.
- Kuna macho ya Kimwili na macho ya kiroho.
- Macho ya kiroho huingia upofu pale ambapo mpira wa tatu( Korodani na uume) unapotumika vibaya na kutolindwa vizuri.
- Macho ya mwili ni mlango wa nafsi. Ni taa na nuru ya mwili wako.
- Lazima uyalinde. Kile unachokuangalia muda mrefu kinaathiri mipira mingine iliyobakia.
- Macho yakiangalia uchafu, ubongo na moyo huchafuka.
- Kuona ni kuamini.
- Macho hujenga Imani ya kweli kuliko Kusikia.
- Ukiona Umaskini sana. Ni lazima utaamini katika umaskini. Na ubongo na moyo wako vitatoa nguvu ya kimaskini.
- Ukiona Matukio ya kikatili. Ubongo na Moyo wako utakuwa na uchungu na utaunda nguvu ya ukatili. Mwishowe utakuwa Mkatili
- Ukitaka uwe tajiri lazima uhisi kama tajiri. Na kuhisi huja kwa kuona.
- Nenda maeneo yenye utajiri, tembea Maeneo walipo matajiri au majumba ya kutajiri. Utaanza kuhisi utajiri ndani yako. Utajiona nawe ni sehemu ya utajiri.
- ukitaka umaskini, nenda au zoea maeneo yenye umaskini na walipo maskini wengi. Kaa kwa muda mrefu. Hisia na nguvu za umaskini vitakuvaa. Lazima utakuwa maskini wewe.
Aiseeh! Nimeandika sana. Naomba nikuage. Kwa neema ya Mungu naamini utakuwa umepata kitu hata kama ni kidogo sana lakini ukikizingatia na kukifuata utaona badiliko chanya katika maisha yako.
Na badiliko hilo ndio Lengo langu. Hiyo ndio itakuwa faida yangu kukuandikia haya.
Acha nipumzike sasa
#DarEsSalaamBusiness #daressalaamtanzania #professoranoldfanue0714577147 !
Comments