Na RichardMwaikenda, Pwani
MGOMBEA Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi CCM Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ameahidi kujenga Reli ya kisasa ya SGR itakayounganisha Bandari kavu ya Kwara na Bandari mpya ya Bagamoyo.
Amesema kuwa endapo wananchi watampa ridhaa ya kuongoza tena nchi kwa kumpigia kura katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29 mwaka huu, Serikali itajenga reli hiyo yenye urefu wa Km.100 ili kurahisisha usafiri wa mizigo kati ya bandari hizo pamoja kongani za viwanda.
Aidha, DKT. Samia ameahidi pia kuanza ujenzi wa Bandari ya kisasa ya Bagamoyo eneo la Mbegani, sambamba na kuanzisha eneo la uwekezaji wa viwanda lenye ukubwa wa zaidi ya ekari 9800.
Ametoa ahadi hizo na nyinginezo katika mkutano wa kampeni za CCM kwenye viwanja vya Sabasaba wilayani Kibaha, Mkoa wa Pwani Septemba 28, 2025.
Comments