Mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Samia Suluhu Hassan, ametoa ahadi nane muhimu kwa wananchi wa mkoa wa Mtwara ikiwa atapewa ridhaa ya kuendelea kuiongoza nchi. Akihutubia wakazi wa mkoa huo, Dkt. Samia alisisitiza dhamira ya serikali yake ya dhati katika Masuala mbalimbali -:


Kwanza, Dkt. Samia ameahidi kuwekeza katika teknolojia ili kuongeza ufanisi katika sekta mbalimbali za maendeleo, huku akisisitiza kulindwa kwa mila na desturi za Kitanzania.


Pili, ameahidi kuboresha sekta ya elimu kwa kuajiri walimu wa kutosha, hususan wa sayansi na hisabati, ili kuinua kiwango cha maarifa kwa wanafunzi na kusaidia taifa kupata wataalamu wa fani mbalimbali.


Tatu, amesisitiza utekelezaji wa mradi mkubwa wa maji wa Nakonde, utakaohakikisha upatikanaji wa maji safi na salama katika wilaya za Mtwara Vijijini na Nanyamba.


Nne, Dkt. Samia ameahidi kuimarisha sekta ya kilimo kwa kuendeleza ruzuku za pembejeo kama sulfa kwa wakulima wa korosho, kukuza mazao mengine ya biashara kama ufuta na mbaazi, pamoja na kuongeza skimu za umwagiliaji na vituo vya ukodishaji wa zana za kisasa.


Tano, ameahidi kutatua migogoro ya ardhi kati ya wakulima na wafugaji kwa kupima na kupanga matumizi ya ardhi, na kuongeza maeneo ya ufugaji kutoka hekta milioni 3 hadi milioni 6 ifikapo 2030.


Sita, amesisitiza kuboresha sekta ya afya kwa kupeleka vifaa tiba vya kisasa na kuajiri wataalamu wa afya ndani ya siku 100 za kwanza za uongozi wake, ili kuboresha huduma za afya kwa wananchi wa Mtwara.


Saba, ameahidi kuendeleza maboresho ya bandari ya Mtwara ili iwe lango kuu la biashara kwa ukanda wa kusini, hasa kwa mazao ya biashara kama korosho na makaa ya mawe.


Nane, amewahakikishia wananchi kuwa serikali yake itaanza ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) kutoka Mtwara hadi Mbambabay, ili kuimarisha usafirishaji wa bidhaa na kuchochea uchumi wa kusini mwa Tanzania.


#bongofmdigital #bongofmupdates

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MBINU ZITAKAZOKUFANYA USIISHIWE PESA

DKT. MIGIRO AKIWASHA KAMPENI ZA DKT. SAMIA MAKAMBAKO

LEO NI LEO KAMPENI ZA DKT. SAMIA SONGWE

NENO KUNTU LA UMMY MWALIMU ALILOLITOA BAADA YA KUTEMWA KUGOMBEA UBUNGE

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

CHONGOLO AMKUMBUKA DKT. ASHA-ROSE MIGIRO-