WAZIRI Mkuu mstaafu na Mratibu wa Kampeni Kanda ya Kaskazini, Frederick Sumaye amesema wasio mtakia mema Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kiama chao ni siku ya Uchaguzi Mkuu Oktoba 29 mwaka huu.
Sumaye ambaye Kanda anayoiratibu ina mikoa ya Kilimanjaro, Arusha na Manyara, ameyasema hayo katika mkutano wa Kampeni za Uchaguzi za CCM mjini Babati leo, Manyara Oktoba 4, 2025
"Kuna watu wanamsemasema Samia, hebu nikumbie anayepigwa vita si Samia ni CCM. Wanaokichukia Chama hicho wako nje ya nchi, miaka yote wanatamani CCM ianguke, Mwalimu Nyerere alisemwa, Mwinyi alisemwa, Mkapa alisemwa, Jakaya Kikwete Magufuli naye alisemwa,"amesema na kuongeza....
....Kwa hiyo kinachotafutwa ni CCM kunguka, sasa walivyoona CCM haitikisiki wakaamua kuhamia kwako mgombea, nakusifu hujamjibu hata mmoja, Sisi Watanzania tutawajibu Oktoba 29."
"Kwa hiyo wananchi tusikiangushe Chama chetu, tuhakikishe tunakwenda kumpigia Samia. wabunge na madiwani wapate majibu yao ili miaka mitano wanyamaze wajipange tena upya kupiga kelele," amemalizia na kuahidi kwamba wananchi wa Manyara watampatia Dkt.Samia asilimia 90 ya kura.
IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA - 0754264203
Comments