▪️Asisitiza kuwa Tanzania na Rasilimali zake zitalindwa kwa gharama yoyote ile.
Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba anazungumza na Wahariri wa vyombo vya habari nchini kwenye kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere, Novemba 25, 2025.
Katika mkutano huo Mheshimiwa Dkt. Mwigulu ametoa wito kwa Watanzania kuwa makini na makundi ya watu wenye nia ya kuichafua na kuiharibu Tanzania.
Mheshimiwa Dkt. Mwigulu amesema kuwa Tanzania ni nchi nzuri hivyo watanzania wanapaswa kuwa makini na wenye nia mbaya na Taifa hili.
Ameongeza kuwa wasioitakia mema Tanzania wanatamani mabaya zaidi yaendelee kutokea, hivyo wawakatae na wasitumiwe kufanya uovu dhidi ya Tanzania “Kila mmoja alibebe jambo hili kwa ukubwa, hawatupendi, wanaangalia rasilimali zetu, nchi yetu sio masikini, kuna watu wanamezea mate rasilimali zetu, ninawahakikishia kuwa tutailinda Tanzania na Rasilimali zake kwa gharama yoyote ile”
Aidha, amesema kuwa kila Mtanzania anapaswa kuwa na dhamira ya dhati na kuunganisha nguvu, katika kulinda na kuitunza Tanzania “tumtangulize Mungu na tuilinde Tanzania, Viongozi wa Serikali katika ngazi zote hakikisheni mnakuwa makini na kila anayeingia kwenye maeneo yenu.
“Hatutaushinda umasikini kama tutaamaini kwamba sekta binafsi ni maadui, Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amebadilisha sheria inayomruhusu mkandarasi mtanzania apate mradi mkubwa na wale wakubwa waombe Sub Contract kwake, hili litatengeneza fursa kwa vijana wa Kitanzania”- Amesisitiza Dkt. Mwigulu.



Comments