Utafiti mpya uliofanywa na gazeti la Daily Mail umebaini kuwa takriban mwanamke mmoja kati ya wawili ana “mpenzi wa akiba” — yaani mtu wa kando ambaye anaweza kuwa chaguo mbadala endapo uhusiano wa sasa hautafanikiwa.
Uchunguzi huu uliohusisha wanawake 1,000 unaonyesha kuwa wapenzi hawa mara nyingi ni rafiki wa zamani aliyeonyesha hisia za mapenzi, mpenzi wa zamani (ex), mfanyakazi mwenzake, au hata rafiki wa mazoezi ya viungo (gym partner). Baadhi ya wanawake wanasema wana uhusiano wa karibu na wapenzi hao kwa zaidi ya miaka saba.
Kinachoshangaza ni kwamba, si wanawake waliopo kwenye mahusiano tu, bali hata baadhi ya wanawake waliopo kwenye ndoa wana wapenzi wa kando kwa kiwango kikubwa zaidi kuliko wale walioko kwenye mahusiano ya kawaida.
Utafiti unaonyesha kuwa baada ya kuachana na mwenza wa sasa, zaidi ya 40% ya wanawake walikutana na wapenzi wao wa akiba na kuanzisha uhusiano mpya, huku asilimia 12 ikikiri kuwa hisia zao kwa wapenzi hao ni kali zaidi kuliko kwa wenza wao wa sasa.
Wengi wa wenza wa sasa wanajua kuhusu uhusiano wa kando, ingawa si wote wanakubaliana au kuufurahia wazo hilo. Utafiti huu unaonyesha kuwa mbinu za kihisia na uwepo wa chaguo mbadala bado ni jambo linalochangia mienendo ya mahusiano katika jamii ya kisasa.

Comments