Miaka mingi iliyopita, eneo ambalo leo linaitwa Kimara au Ukanda wa Gaza lilikuwa ni njia ya wasafiri kuelekea maeneo mengine, lakini lilikuwa na misitu mikubwa, wanyama wakali, na hatari nyinginezo za kila aina.
Kulikuwa na mzee mmoja jasiri kutoka Mkoa wa Mara, aliyejulikana kama Mzee Maratu akiishi Maeneo hayo
Km mnavojua watu wa Mara walijulikana tangu zamani kwa ujasiri wao, nguvu za kupambana na mazingira magumu, hawakuwa na hofu ya changamoto. Mzee Maratu pia alikuwa na sifa hizi.
Alikuwa shupavu, mtu aliyejua jinsi ya kuishi na pori, na alikabiliana na kila hatari kwa busara na nguvu. Alijua namna ya kupambana na wanyama wakali na vibaka waliokuwa wakivizia njiani.
Wasafiri walipopita Maeneo hayo waligundua kuwa Mzee Maratu ndiye aliyewezesha wengi kupita salama katika sehemu hii yenye hatari. Hivyo, walikuwa wakiita eneo hilo kwa shauku:
“Twende kwa yule Mzee wa Mara… kwa Ki-Mara!”
Baada ya muda, jina hili likaanza kubadilika kidogo kidogo, likawa rahisi kutamkwa, na hatimaye likapata jina la Kimara.
Hivyo, jina hili lilibeba alama ya ujasiri, nguvu, moyo usioogopa, na roho ya kujitolea.
Kimara si jina tu, bali ni kielelezo cha nguvu za kupambana na mazingira magumu, Ushupavu na kujjitolea kusaidia wengine.
Leo hii, unaweza kusikia majina mengi ya Kimara kama vile:
Kimara King'ongo, Kimara Bucha, Kimara Kona, Kimara Baruti, kimara korogwe n.k
#jamiidiary
#makala #article

Comments