Watu wengi hudhani familia ya Mbowe na familia ya Mwalimu Nyerere ni maadui, Kwasababu tu kuwa Freeman Mbowe ni mpinzani sio kweli.
Familia hizi ni familia marafiki sana tokea enzi za Mwalimu Nyerere mpaka leo ninavyokuletea makala hii na zina heshimiana sana lakini pia usichokijua ni kwamba, Freeman Mbowe humchukulia Mwalimu Nyerere kama baba yake.
Siyo kwamba humchukulia kama baba kwasababu, Mwalimu Nyerere ni Baba yetu wa Taifa tu hapana, Humchukulia kama baba yake kwasasababu ya urafiki mkubwa uliokuwepo kati ya baba yake mzazi na Mwalimu Nyerere.
Unae muona hapo pichani anae peana mikono na mwalimu Nyerere ni baba yake mzazi na Freeman Mbowe, Kwa wale musiomjua Kwa jina anaitwa Aikael Alfayo Mbowe, Picha hiyi ilipigwa huko mkoani kimanjaro, Wakati Mwalimu Nyerere alipokuwa anafanya ziara mkoani humo.
Mzee Aikael Alfayo Mbowe alikuwa ni tajiri mkubwa mkoani Kilimanjaro, Aliyetoa mchango wa kipekee kwa chama cha TANU ikiwemo kuwashawishi na kuwaingiza wananchi wa Arusha na Kilimanjaro, Kwenye chama cha TANU wakiwemo machifu,
Kiufupi mzee Mbowe ni moja ya wapigania uhuru wakubwa hapa nchini, Kutokana na kitendo hicho Mwalimu Nyerere alimpenda sana mzee Aikael Alfayo Mbowe, Hatimae wakawa marafiki wakubwa wakati wa uhai wao naa ilifika hatua mzee Aikael Alfayo Mbowe akawa akitaka kwenda Ikulu anaenda muda wowote Kumuona Mwalimu Nyerere na kuzungumza nae,
Mzee Aikael Alfayo Mbowe ndio mzee aliekwenda Ikulu mara nyingi zaidi kuliko mzee yoyote enzi za Mwalimu Nyerere akiwa Ikulu na mara nyingi alipokua akienda alikua anaenda na mwanawe aitwae Freeman Mbowe naa hapo ndipo ilipozuka dhana kuwa Freeman Mbowe amelelewa Ikulu,
Urafiki wa Mwalimu Nyerere na mzee Aikael Alfayo Mbowe, Ulisababisha hata familia zao ziwe na urafiki wakubwa, Kama ulikua hujui ni kwamba Freeman Mbowe na Makongoro Nyerere.
Mwaka 1983 mtoto wa mwalimu Nyerere, M!akongoro alipotaka kuoa, Mzee Aikael Alfayo Mbowe ndie alikua mshenga katika ndoa yake.
Wakati Freeman anabatizwa 9/12/1961, Siku ambayo uhuru wa nchi hii ulipatikana, Aliekuwa baba wa ubatizo ni mwalimu na hata jina "Freeman" alilitoa mwalimu mwenyewe.

Comments