Sio maneno ya kukatisha tamaa — ni maneno ya kukufungua macho.
Huu ndiyo ukweli ambao wengi wanaukwepa, wanaficha, au wanauchukulia kama mashambulizi…
Lakini ni ukweli unaoumia kama sindano, ila unaponya kama dawa.
01. Wengi Hawana Pesa — Sio Kwa Sababu Hakuna Fursa… ila kwa Sababu Hakuna NIDHAMU.
Gen Z wanapenda matokeo ya haraka.
Lakini hawataki:
kujifunza skill
kustahimili maumivu
kuanza na sifuri
kukaa chini mwaka mmoja bila kuona matokeo
kujengea uwezo polepole
Wanataka “lifestyle”, hawajui “lifestyle” huja mwishoni.
02. Maisha ni MAGUMU — Lakini Hakuna Atakayebadili Maisha Yako Zaidi ya Wewe Mwenyewe.
Myles Munroe alisema:
> “Ulimwengu hautaki maelezo yako, unataka thamani yako.”
Gen Z wengi wanataka huruma.
Wanataka kueleweka.
Wanataka kusikilizwa.
Lakini dunia inataka “utupe kitu” kabla haitakupa chochote.
03. Wamesoma Ila Hawana Kazi — Kwa Sababu KAZI SIKU HIZI NI SKILLS, SIO CERTIFICATE.
Degree ni chombo.
Skill ni silaha.
Na siku hizi dunia inatafuta wapiga kazi, sio wenye karatasi.
Kwa Tanzania leo:
Mhitimu mwenye social media skill anapata 600k–1M
Mhitimu asiyejua kompyuta anangoja ajira miaka 5
Ukweli mchungu:
CV bila skill ni kama simu bila charge. Inaonekana nzuri lakini haina kazi.
04. GEN Z Wanajiona “Special” Lakini Hawajafanya Kitu Kinachowafanya Wawe Special.
Wana mindset ya:
“Nitafanikiwa tu”
“Nitapata kazi tu”
“Nitapata connection tu”
Hakuna tu kwenye maisha.
Hakuna guarantee.
Unatakiwa ujitegemee, sio ujiari.
05. Wengi Wanataka Pesa Kubwa Lakini Hawako Tayari Kufanya Kazi Kubwa.
Ukweli mchungu:
Kiwango cha kipato ni sawa na kiwango cha uwezo uliojengea thamani sokoni.
Kama ujuzi wako ni wa kawaida → kipato chako kitakuwa cha kawaida.
Kama ujuzi wako ni rare → kipato chako kitakuwa rare.
06. Wengi Wanailaumu Serikali, Familia, Elimu… Lakini Hawajawahi Kujiuliza: “Mimi nimefanya nini?”
Jim Rohn alisema:
> “Don’t blame the wind. Adjust your sails.”
Wengi wanaishi kwa excuses:
“Nilizaliwa maskini.”
“Nimesoma vibaya.”
“Hakuna connection.”
“Serikali inaninyima ajira.”
Lakini mtu wa ukweli huanza na alicho nacho.
Sio alichonyimwa.
Mwl Kennedi Masawe ..✍️

Comments