CHIMBUKO LA WACHAGGA NI KUTOKA ETHIOPIA

Chimbuko na Asili ya kabila la wa Chagga inaonesha kuwa walitokea Afrika Kaskazini upande wa Mashariki mwa Afrika yaani pande za Ethiopia/Uhabeshi na wakaendelea kusambaa chini hadi Kenya na kufika hadi ukambaa. 

Wakaendelea kusambaa zaidi kusini mwa Kenya na kusukumizwa hadi Kilimanjaro.

 Wachaga au Walawi hawa walipofika Kilimanjaro walikuta watu wadogo sana waliokuwa wakiishi hapo au wenyeji wa hapo yaani vimbilikimo au wambuli au vibete au iwakonyigo hawa wana majina mengi sana.

 Wachaga hawa walikuwa na mifugo mingi sana yaani ilikua ni kundi kubwa la wachaga wakihama na kuweka makao yao hapo Kilimanjaro.

 Vimbilikimo hivyo walipowaona watu hao wakubwa kuliko wao waliondoka na kuogopa na wakaenda upande wa Kongo yaani walikimbilia misitu ya Kongo.

 Kipindi wakoloni walipofika Kilimanjaro waliwaita walawi hao chaka sababu walitengeneza vibanda vya mifugo yao vichakani ndipo baadae wakaitwa chaga.

 Sababu nyingine ya wachaga kufika hapo Kilimanjaro ni kutafuta malisho. 

Baadae sana wachaga walikua na umoja na mafanikio makubwa kabla hata ya uhuru na ilikua watengeneze serikali yao.

 Wazungu walipo panga njama za kuligawa bara la Afrika yaani scramble for Africa au Rape of Africa walitumwa watu na wawakilishi waanze kazi hiyo.

 Walipokuja Tanganyika walikuta wabantu wana serikali yao na ustaarabu wao na walikuta tawala zenye nguvu na mfumo rasmi, moja wapo ikiwa ni tawala na dola la kichaga yaani Chaga State na kiongozi wao Mangi Mkuu au Mfalme mkuu.

 Ikumbukwe pia wachaga kiasili ni walawi, kulikua na makabila 12 moja ya kabila ndilo hilo walawi ambao baadae waliitwa chaga toka neno chaka na wakoloni hadi leo. 

Chimbuko la makabila matatu ambayo ni Wameru, Wamaasai na Wachaga ambao Baba yao wa asili alikua Lawi wa Biblia Kutoka 6:19, 1Nyakat6:19, 24:30 Na wana wa Merari ni Mali na Mushi, hizi ni jamaa za hao Walawi kulingana na vizazi vyao. 

1 Mambo ya Nyakati 9:12 na Adaya, mwana wa Yerohamu, mwana wa Pashuri, mwana wa Malkiya; na Maasai..


 

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

VITU 10 WANAUME WANAVYOPENDA ZAIDI TOKA KWA MWANAMKE — SIYO SURA, SIYO MWILI ❤️

WALIOCHUKUA FOMU CCM ZA KUWANIA USPIKA HAWA HAPA

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HUYU NDIYE WANU HAFIDH, CHAMPIONI WA ELIMU

UKWELI KUHUSU TENDO LA NDOA NA FAIDA ZAKE

MAWAZIRI WALIOACHWA HAWA HAPA

HISTORIA YA MAREHEMU MC PILIPILI

USIKUBALI KUWA LOFA KWA MWANAMKE...