.1. Anakuomba sana pesa.
Ushakuwa na yule demu ambaye mazungumzo ya wewe na yeye huwa yanahusu pesa mara nyingi, yani akipiga simu ni pesa, ukiona tu ujumbe wake unajua hapa inahitajika pesa, kila kitu ni pesa, hana huruma na wewe kuhusu pesa.
-Mwanamke wa hivi hana upendo na wewe hata kidogo, mwanamke anayekupenda kweli na ana malengo na wewe haombi pesa kwa namna hiyo, hakuombi pesa kama ana kukomesha, na upo muda ukikwama anakusaidia lakini kwa mtu asiyekupenda yeye anakuomba hela vibaya mno.
2. Unatumia nguvu kubwa sana unapohitaji kukutana naye.
Huwa nawaambia vijana wa kiume kila siku na leo nawakumbusha, hakuna mwanamke ambaye yupo busy kwa mwanaume anayempenda, utampata muda wowote unaomuhitaji bila kutumia nguvu yoyote ile.
-Tambua kwamba kipindi wewe unambembeleza kwa nguvu kubwa muonane, wakati huo huo yeye anamuomba mwanaume anayempenda amruhusu aende kwake.
3. Mara zote mlizokutana, ni wewe ndiye uliomba mkutane.
Una mwanamke, lakini huyo mwanamke hajawai hata siku moja kukwambia anakuja kwako, yani yeye kuja kwako lazima umuite, hiyo ni changamoto.
-Wanawake wanapenda sana kutulia magetoni kwa wanaume wanaowapenda, mara nyingi ni yeye ndio atakuwa anakwambia anakuja, na ukimwambia leo sipo atalaumu sana.
4. Anakufokea.
Ulishakuwa na demu ambaye yani hata kitu kisichoeleweka anakufokea, yani mnaweza tu kuwa mnaongea labda ukamuuliza kitu unaona anaanza tu kufoka, kwahiyo mzee kaka inabidi ushuke chini mamaa apoe, aisee ondoka kwa hiyo manzi, no love there.
5. Hataki umtambulishe kwa watu wako wa karibu na wala yeye hakutambulishi kwa watu wake.
Ukweli ni kwamba mwanamke anayekupenda anajisikia vizuri zaidi anapotambulishwa kwa watu wa karibu au ndugu za mpenzi wake.

Comments