GEORGE AFICHUA UTAJIRI MKUBWA WA MANGE KIMAMBI ANAOUPATA KUICHAFUA TANZANIA


Mange Kimambi, mwanamitindo aliyebadilika kuwa mwanaharakati wa siasa, ndie muasisi wa maandamano kadhaa yaliyofeli nchini Tanzania, akiyaitisha kupinga kile anachokiita kuwa ni muendelezo wa ukiukwaji wa haki za binadamu na uminywaji wa haki za kiraia nchini Tanzania. 

Katika mtazamo huo amefanikiwa kuwarubuni maelfu ya wananchi ambao mara kadhaa wamemuona kama mtetezi wa kweli bila kuufahamu ukweli na maslahi binafsi anayoyapata Mange Kimambi pale anapofanikiwa kuwavurugu na kueneza chuki kwa Watanzania aidha kwa serikali yao ama kwa watu mashuhuri na Viongozi kadhaa.

Kulingana na Mchambuzi George Josephat, anamtaja Mange kama Miongoni mwa 'Diaspora' tajiri sana kutoka Barani Afrika, utajiri wake ukitokana na makampuni na Mashirika ambayo yamekuwa yanachimba madini nchini pamoja na kuendesha miradi mikubwa ya Kimkakati.

Fedha hizi na ubia kati yake na Makampuni hayo zilikoma pale Hayati Dkt. John Pombe Magufuli, enzi za uhai wake alipositisha Mikataba na Makampuni hayo, mengi yakiwa yametokea kwenye Mataifa ya Umoja wa Ulaya na Amerika.

"Hapa ndipo Mange Kimambi alipoanza kutumika na mabeberu. Lengo likiwa ni kuonesha majaribio ya kuundoa ama kuusumbua utawala uliokuwepo hadi pale watakaporejesha Mikataba ili Wafadhili wake hao waweze kurudi katika mifumo ya kutafuna rasilimali za Tanzania kwa maslahi kiduchu waliyokuwa wakilipa kwa serikali." Amesema Bw. George.

Kulingana na Mchambuzi huyo,  kwa makadirio ni kuwa ndani ya Mwezi mmoja, Mange Kimambi alikuwa akiingiza wastani wa dola 35, 420 sawa na takribani Shilingi Milioni 87, 133, 200 kwa kazi hiyo tu ya kujaribu kushinikiza Makampuni hayo kurejeshwa kwenye mfumo.

Bahati mbaya ni kuwa wakati anafanya harakati hizo, alikuwa akijificha nyuma ya uzalendo, mpenda nchi na mwenye uchungu na rasilimali za Taifa, suala ambalo likasababisha kupata wafuasi wengi na ambao wameendelea kutumika mpaka leo kutekeleza ajenda zake mbalimbali ambazo yeye binafsi amekuwa akilipwa mamilioni ya fedha na kuwaacha Watanzania kati



 

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

UKWELI KUHUSU TENDO LA NDOA NA FAIDA ZAKE

HUYU NDIYE WANU HAFIDH, CHAMPIONI WA ELIMU

MAWAZIRI WALIOACHWA HAWA HAPA

VITU 10 WANAUME WANAVYOPENDA ZAIDI TOKA KWA MWANAMKE — SIYO SURA, SIYO MWILI ❤️

๐Œ๐‰๐”๐„ ๐Š๐€๐‚๐‡๐„๐‘๐Ž ๐Œ๐™๐„๐๐€

HISTORIA YA MAREHEMU MC PILIPILI

USIKUBALI KUWA LOFA KWA MWANAMKE...

NAPE AWAPA UKWELI VIJANA