KAULI NZITO ZA NIFFER BAADA YA KUACHIWA HURU




Mfanyabiashara na kijana Niffer Jovin ametoa kauli yake ya kwanza hadharani baada ya kuachiwa, akieleza kuwa kipindi alichopitia kimempa tafakari pana kuhusu nafasi ya vijana katika kufanya maamuzi, hasa pale mihemko inapokuwa juu kuliko busara.

Niffer amesema kuwa kupitia tukio hilo amejifunza umuhimu wa kutafakari kwa kina kabla ya kuchukua hatua yoyote, akibainisha kuwa sehemu kubwa ya ushiriki wake katika matukio ya vurugu ilikuwa ni matokeo ya mihemko ya ujana, si uchambuzi makini wa kinacho Endelea.

Amesema kuwa wakati wa vurugu mbali mbali, kuna watu wengi ambao hawakupata haki zao kwa wakati kwa sababu ushahidi muhimu kupatikana ulikuwa mgumu kutokana na hali ya sintofahamu iliyokuwa imetanda. Kwa mujibu wake, hali hiyo imefanya atambue kuwa vurugu huathiri sio tu wanao shiriki, bali hata watu wasio kuwa na hatia ambao hupoteza haki zao kwa kucheleweshwa kufikishwa au kusikilizwa mahakamani kwasababu ya vurugu.

Niffer ameonya vijana wenzake dhidi ya kujitumbukiza katika vitendo vya fujo bila kuelewa athari zake pana, akisisitiza kuwa mihemko bila fikra inaweza kusababisha maumivu makubwa kwa mtu binafsi, familia na jamii pana. Amesema kuwa maumivu na changamoto alizopitia zimemsaidia kuona utofauti kati ya uamuzi sahihi na uamuzi wa hasira.

Kwa unyenyekevu, amekiri makosa yake na kueleza kuwa amejifunza somo muhimu ambalo angependa vijana wengine walitambue mapema

Hakuna sababu ya kuhatarisha maisha au mustakabali kwa kushawishiwa na hisia za muda mfupi.

Mwisho, ametoa wito kwa vijana kote nchini kujiepusha na vitendo vinavyo hatarisha usalama na kuvuruga utaratibu wa kisheria, akihimiza kujenga misingi ya mazungumzo, utulivu, na kufanya maamuzi yenye tafakuri na busara.

Mwisho kabisa amemshukuru Mwenyezi Mungu Pia Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa Msamaha aliotoa pia Amewashukuru watanzania wote kwa jumla walio muombea.

Alimaliza kwa kusema watu wapeleke misaada magerezani kama Taulo za kike na mavazi.

Nyongeza ya Mchambuzi Profesa Chotara Mweusi Sultan πŸ‘‡

πŸ‘‰Mwenyezi Mungu Atujalie Kheri wanadamu wote na atuepushe na kila aina ya Baya Atuweke kando na Mihemko inayoweza kugharimu maisha Yetu na kuacha simanzi kubwa katika Familia zetu na Jamaa zetu.


 

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

VITU 10 WANAUME WANAVYOPENDA ZAIDI TOKA KWA MWANAMKE — SIYO SURA, SIYO MWILI ❤️

WALIOCHUKUA FOMU CCM ZA KUWANIA USPIKA HAWA HAPA

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HUYU NDIYE WANU HAFIDH, CHAMPIONI WA ELIMU

UKWELI KUHUSU TENDO LA NDOA NA FAIDA ZAKE

MAWAZIRI WALIOACHWA HAWA HAPA

HISTORIA YA MAREHEMU MC PILIPILI

USIKUBALI KUWA LOFA KWA MWANAMKE...