Staa wa Yanga SC, fundi wa mpira Pacome Zouzou, ametoa kauli ya kushangaza kwa mashabiki wa soka baada ya kusema wazi kupitia tiktok live kuwa hana ndoto ya kucheza Ulaya, akibainisha kuwa kwa sasa anafurahia zaidi maisha yake ndani ya Yanga.
Pacome amesema kuwa lengo lake kubwa si kusaka nafasi barani Ulaya kama ilivyo kwa wachezaji wengi wa Kiafrika, bali anapita katika kipindi kizuri cha maisha na soka lake akiwa Yanga kipindi ambacho hakioni kama anapaswa kukikimbia.
Ameeleza kuwa mazingira ya klabu, mapenzi ya mashabiki, na namna anavyopewa thamani ndani ya timu vinamfanya ajisikie kuwa nyumbani, jambo linalompa nguvu na uhuru wa kucheza kwa kiwango cha juu.
Kauli ya Pacome imeibua mjadala mitandaoni, mashabiki wengine wakimupongeza kwa uaminifu na kujitoa kwake, huku wengine wakiona uwezo wake ungemruhusu kucheza katika ligi kubwa zaidi.
Hata hivyo, Pacome amesisitiza kuwa kwa sasa anajikita kikamilifu katika mafanikio ya Yanga na kutimiza malengo ya klabu ndani ya msimu huu.
๐ฐ
Comments