Waziri wa Mambo ya Ndani, George Simbachawene amemuagiza Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Camillus Wambura, kuhakikisha ukamataji wa Watu unafuata taratibu za kisheria na amepiga marufuku Polisi kuwakamata Watu kibabe wakiwa wamevaa kininja, wakiwa bila sare na silaha kubwa. Akiongea Jijini Dar es salaam leo December 08,2025.
““Nimemuelekeza IGP kwamba katika kipindi hiki kwakweli nisingependa ukamataji wa tofauti, ukamataji ninaoupenda Mimi ni ule wa kwa mujibu wa sheria, Askari amevaa sare anakwenda kuripoti kwamba Jeshi la Polisi kuna Mtu tunamuhitaji, tunataka kwenda kumuhoji tunataka kumchukua, basi anagongewa yule Mtu anachukuliwa tena mchana, kwasababu yule Mtu yupo, anajulikana kazin kwake ana anafanyia shughuli zake wapi, yanini uende ukamkamate nyumbani kwake, Watu wamevaa ninja, hawana sare, masilaha makubwa makubwa, tumekubaliana huu ukamataji hapana”
“Tunataka ukamataji ambao Wananchi wetu wameuzoea wenye staha, hatutaki Mtu akikamatwa hata Watoto wake wapate hofu pale nyumbani, yanini kupeleka hofu hadi kwa Watoto?, unaiacha ile trauma yule Mtoto atakuwa anachukia Polisi tu akiwaona Polisi anasema walimkamata Baba hao, walimkamata Mama, Mimi nadhani ukamataji mzuri ni ule wenye staha”
“Huo ukamataji mwingine tofauti na hivyo tumekubaliana, sio kosa dogo tu Mtu amepost kakitu kadogo tu unasema uchochezi huo, hii hapana, nadhani na lenyewe limechochea baadhi ya Watu kuwachukia Polisi lakini Polisi hawahawa ndio wanafanya mtaani tunaishi kwa usalama”

Comments