UKIONA NCHI YA KIZUNGU INAFOKEWA NA NCHI YA AFRIKA USISHANGAE MAMBO YAMEBADILIKA.


Fuatana nami Mchambuzi wako Profesa Chotara Mweusi Sultan.

Ulimwengu wa Afrika upo katika Mabadiliko ya Kimkakati kwa Sasa jambo linalo Ilazimu Magharibi Kuondoka bila kupenda Afrika. 

Kwa lugha Laini ni kwamba Ushawishi wa magharibi Afrika ndio unatokomea taratibu taratibu hivo, Mambo yalianza kama utani ila kwasasa Afrika imeungana katika Kuwakataa Wamagharibi.

Tukianza na Ukanda wa Sahel Yani Nchi za Mali, Niger, Burkina Faso, Chad, Mauritania Tayari Wamagharibi wameondoka Rasmi kijeshi na kwa Ushawishi wao, Kwa Ufupi hawana cha Kuongea na kikatekelezwa Mbele ya mataifa Hayo.

πŸ‘‰Kupungua kwa ushawishi wa Magharibi, Marekani na Ufaransa awali walitumia nguvu za kijeshi na kitu walicho kiita misaada ya maendeleo japo si misaada bali ni Mikopo kudhibiti hali ya usalama.

Sasa, mataifa haya yana jitegemea zaidi kwa ushirikiano wa kikanda (ECOWAS) na ushirikiano wa Russia, China na Iran).

πŸ‘‰Kukataliwa kwa msaada wa kijeshi wa moja kwa moja wa Ufaransa Kunafungua Njia ya Ushirikiano wa mataifa ya Asia katika uwekezaji na mikopo ya maendeleo katika Ukanda huo.

πŸ‘‰Tukija pia Ukanda wa Kusini mwa Afrika Yani Nchi za Namibia, Botswana, Zimbabwe, South Africa na Zambia

Mataifa haya, yana biashara ya moja kwa moja na China, India, UAE na Iran, jambo linalo punguza utegemezi wa Marekani na EU.

Umoja wa SADC unaongeza ushawishi wa kikanda na kupunguza mgongano wa kigeni.

πŸ‘‰Mikopo ya kifedha ya EU na USA si chimbuko pekee la maendeleo, Mashirika ya kigeni kutoka Asia hutoa mbadala wa uwekezaji.

Hali inazidi kua Mbaya kwa Wamagharibi kulingana na vuguvugu hilo kuingia Rasmi Ukanda wa Afrika Mashariki Yani Nchi za Tanzania, Kenya, Uganda, Burundi, Rwanda na Ethiopia

πŸ‘‰Ukweli ni kwamba Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) inakuza ushirikiano wa kikanda katika biashara, elimu, na Usalama, Ili kupunguza udhibiti wa Magharibi.

Uwekezaji kutoka China (mfanoπŸ‘‰ Reli ya Standard Gauge Railway Kenya na Tanzania) na UAE unazidi kuonekana.

Mikopo ya maendeleo au shinikizo la kisiasa kutoka Magharibi sasa linashindwa Kua Kauli ya mwisho kila Panapo Kucha.

πŸ‘‰Mataifa ya kiafrika yana pendelea uhusiano wa kibiashara wa moja kwa moja badala ya utegemezi wa Mikopo.

πŸ‘‰Ndio mana Uliona Umoja wa Afrika (AU) Ulitoa tamko la kuwafokea Bunge la Ulaya Pindi lilipo thubutu kuingilia mambo ya ndani ya Tanzania kwa kile kilicho tokea October 29, Hii Inadhihirisha kwamba Jamaa wanazidi kupoteza Nguvu zao katika Mataifa ya Afrika.

Hivi ni Vigezo vya Pamoja Vinavyo sababisha Kupungua kwa Ushawishi wa Magharibi Hapa Afrika πŸ‘‡

πŸ‘‰Uchumi unao jitegemea Uzalishaji wa mali ghafi, biashara na uwekezaji wa Asia
Ushirikiano wa kikanda Jumuiya za kikanda Yani πŸ‘‰ (SADC, EAC, ECOWAS) zinaunda nguvu ya pamoja.

Biashara ya kigeni isiyo ya Magharibi yani China, India, UAE, Iran zinatoa mbadala wa kiuchumi, Ujasiri wa kisiasa.

Viongozi wa Afrika wana sera za kujitegemea na kushindwa kukabiliwa na shinikizo la Magharibi. Teknolojia na media Yani Mitandao inapanua ufahamu wa wana nchi wa Afrika na kupunguza propaganda za Magharibi

Hivo basi πŸ‘‰ Magharibi Hapo Awali walidhibiti kwa nguvu za kijeshi, mikopo ya kifedha, na shinikizo la kisiasa.

Kwa Sasa πŸ‘‰Africa inajitegemea kijiografia, kiuchumi, na kisiasa, huku ikitumia mbadala kutoka Asia na Umoja wa Kikanda katika maswala ya kijeshi.

Ushawishi wa Magharibi umepungua hatua kwa hatua katika ukanda wote wa:

πŸ‘‰Sahel
πŸ‘‰Mashariki ya Afrika 
πŸ‘‰na Kusini mwa Afrika.

Japo kuna nchi bado ziko pamoja na magharibi lakini Nyingi zenye Ushawishi zimeikataa Magharibi, Kwahiyo ukiona Nchi ya Afrika ikiifokea nchi yoyote ya kizungu usishangae Zama zimebadilika Sio kila homa ni Malaria zingine ni U.T.I.

Afrika tunayo ihitaji ndio hii Afrika ya Sasa, Tunahitaji kujiamulia mambo yetu na sio Kuamuliwa na Watesi wetu, Ukweli ni kwamba Makubwa zaidi yanakuja kuhusu Afrika kujikomboa kwa Mabeberu.

Baki na Mimi kwa Mengi zaidi yanayo jiri Duniani 

By Professor Chotara Mweusi Sultan kutoka viunga vya πŸ‘‡ 
πŸ‘‰Sharif shamba 
πŸ‘‰Ilala Dar es salaam 
πŸ‘‰Tanzania 

Bingwa la uchambuzi wa maswala ya kijamii, Uchumi na Siasa za Dunia Yetu.


 

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

VITU 10 WANAUME WANAVYOPENDA ZAIDI TOKA KWA MWANAMKE — SIYO SURA, SIYO MWILI ❤️

WALIOCHUKUA FOMU CCM ZA KUWANIA USPIKA HAWA HAPA

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

UKWELI KUHUSU TENDO LA NDOA NA FAIDA ZAKE

HUYU NDIYE WANU HAFIDH, CHAMPIONI WA ELIMU

MAWAZIRI WALIOACHWA HAWA HAPA

HISTORIA YA MAREHEMU MC PILIPILI

USIKUBALI KUWA LOFA KWA MWANAMKE...