MASHABIKI SIMBA, YANGA WATAMBIANA AZANIA BUNGE BONANZA

Mashabiki wa Klabu za Simba na Yanga wametambiana kwamba wataoneshana ubabe katika mashindano ya Azania Bunge Bonanza 2026 litakalofanyika kwenye viwanja vya St Merlin Miyuji jijini Dodoma Jumamosi Januari 31, 2026.

Tambo hizo zimefanyika wakati wa mkutano na vyombo vya habari kwenye Ukumbi wa Bunge wa Pius Msekwa jijini Dodoma leo Januari 29, 2026 ambapo Benki ya Azania wadhamini wa bonanza hilo wamekabidhi vifaa vitakavyotumika kwa Mwenyekiti wa Bunge Bonanza, Festo Sanga. Vifaa vya michezo vilivyokabidhiwa ni; jezi, suti za michezo, mipira na medali mbalimbali.

Mgeni rasmi katika bonanza hilo anatarajia kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Nchemba. 

Michezo itakayo shindaniwa katika katika bonanza hilo litakaloanza kwa matembezi yatakayoongozwa na Waziri Mkuu, kutoka Chuo cha Mipango hadi St. Merlin ni; soka,netibali, wavu, mpira wa kikapu, mbio, kukimbia kwenye magunia, kukimbiza kuku , kula wali, kunywa soda, bao, drafti na mingineyo.

Bonanza hilo litashirikisha wabunge mashabiki wa vilabu hivyo, watumishi wa bunge, watumishi wa Benki ya Azania na taasisi nyingine pamoja na wanamichezo mbalimbali.

Washindi watapatiwa zawadi mbalimbali zikiwemo  medali na vikombe.

 Mwenyekiti wa Bunge Bonanza, Festo Sanga (aliyevaa kaunda suti katikati) akiwa na mashabiki wa Yanga na Simba.
Viongozi wa Benki ya Azania wakikabidhi vifaa mbalimbali vya michezo kwa Sanga.








 

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

MIKOA 10 YENYE KIPATO KIKUBWA ZAIDI KWA MTU MMOJA MMOJA

BODABODA ALIPWA PIKIPIKI BAADA KUSAFIRI KWA BODA KWA SAA 10 MBEYA HADI DAR

ASANTE GWIJI YAYA TOURE KWA KUPASUA UKWELI UKWELI KUPENDELEWA KWA MOROCCO

CONFIRMED HAWA NDIO WACHEZAJI WETU 12 WA KIGENI 🦾

'MAREKANI IKIJARIBU KUANZISHA VITA NA URUSI ITAANGAMIA'

RAIS WA SENEGAL AWAPATIA ZAWADI NONO WACHEZAJI WALIOFANIKISHA UBINGWA WA AFCON 2025

NYOMI YA WASENEGALI WAKISHANGILIA UBINGWA WA AFCON 2025