Leo jioni nimewasili Dubai, Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) ambapo nitaungana na viongozi wengine katika uzinduzi wa Global Africa Investment Summit (GAIS) pamoja na Mkutano wa Dunia wa Serikali (World Governments Summit - WGS) 2026 unaolenga kujenga mwelekeo wa namna serikali zinavyoweza kuhimili mabadiliko ya dunia na kuchochea maendeleo endelevu.
Ushiriki wa Tanzania katika majukwaa haya ni kielelezo cha uthabiti wake kisiasa, na dhamira yake ya kuendelea kuvutia uwekezaji toka ndani na nje ya nchi, utakaozalisha ajira zaidi na kuchagiza maendeleo yetu. Aidha, ni utekelezaji wa Dira 2050 pamoja Sera mpya ya Mambo ya Nje katika Diplomasia ya Uchumi. NA IKULU. @Khamisi Mussa.



Comments