Na Richard Mwaikenda, Dodoma
Waziri Mkuu mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mizengo Pinda ameongoza kupanda miti 1000 katika eneo la Ndejengwa jijini Dodoma leo Februari 6, 2026.
Katika shughuli hiyo iliyoandaliwa na Taasisi ya Habari Conservation,Mzee Pinda ambaye ni mlezi wa taasisi hiyo aliongozana na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule ambaye pia alipanda mti wa kumbukumbu.
Pia walishiriki wanafunzi na wananchi wanaoishi karibu na eneo hilo wazi ambalo kwa mujibu wa Afisa Habari wa Taasisi hiyo, Loyce Joseph amesema wataligeuza kuwa msitu wenye miti ya kivuli na matunda jambo ambalo litakuwa linavutia watu kwenda kutembelea na kufanya sherehe zao ndogo ndogo.
Shughuli hiyo imedhaminiwa kwa asilimia kubwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA) ambayo Mkurugenzi wake Mkuu ni CPA. Dennis Simba ambaye pia yeye na watumishi wake walishiriki kupanda miti.
Mzee Pinda, na Mkuu wa Mkoa Senyamule wameipongeza taasisi hiyo inayoongozwa kwa asilimia kubwa na waandishi wa habari, kwa kuwa mstari wa mbele kuijakinisha Dodoma.
Pinda akipanda mti.
RC Senyamule akipanda mti huku akisaidiwa na Mzee Pinda. Katikati ni Mwenyekiti wa Taasisi hiyo, Bernard James.
Mkurugenzi wake Mkuu ni CPA. Dennis Simba akipanda mti.
Bosi wa PPRA Simba akielezea kuhusu udhamini wa shuguli hiyo.
Baadhi ya wananchi jirani na eneo hilo walioshiriki kupanda miti.
Mzee Pinda akizungumza baada ya kupanda miti na kushauri kuandaa utaratibu maalumu wa kuwashirikisha vijana kupanda miti.
Mmoja wa wanafunzi akielezea jinsi walivyoshiriki kupanda miti ili kutunza mazingira.
Viongoi wakiwa katika picha ya pamoja na wanachama wa Taasisi hiyo.
Wakiwa na baadhi ya wanafunzi walioshiriki kupanda miti.
Akifungua moja ya mabomba ya maji maalumu kwa uwagiliaji wa miti katika eneo hilo.
Afisa Habari wa Taasisi hiyo, Loyce Joseph akipanda mti.










Comments