EID EL FITR NI LINI? MAMBO 10 ANAYOPASWA MUISLAMU SIKU HIYO

 

Eid El-Fitri ni miongoni mwa sikukuu kubwa na zenye heshima kubwa katika Uislamu, ikija mara moja kila mwaka baada ya kukamilika kwa mwezi mtukufu wa Ramadhani. Ni siku ya furaha, shukrani na mshikamano kwa Waislamu duniani kote baada ya mwezi mzima wa ibada, kujinyima na kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu.

Katika siku hii muhimu, Waislamu husherehekea kwa nyoyo zilizojaa furaha, wakikumbuka mafanikio ya kufunga na kufanya ibada mbalimbali. Pia ni wakati wa kuimarisha mahusiano ya kifamilia na kijamii kupitia ziara, sadaka na kushirikiana chakula.

Kwa wengi, Eid ni zaidi ya sherehe; ni siku ya kuonesha ucha Mungu, upendo na mshikamano kwa jamii. Watu huvaa nguo nzuri, kuandaa vyakula maalum na kuwakaribisha ndugu, jamaa na marafiki.

Hata hivyo, pamoja na furaha yake, siku ya Eid pia ina taratibu na mambo muhimu ambayo Muislam anapaswa kuyazingatia ili kuhakikisha anaitimiza kwa mujibu wa mafundisho ya dini ya Kiislamu.

Eid ni Lini?Kuna maeneo hutumia vyombo kama hivi kuutafuta mwezi 

Nchi kadhaa za Ghuba zikiwemo Saudi Arabia, UAE, Qatar, Kuwait na Bahrain zimetangaza leo asubuhi tarehe ya Eid al-Fitr 2026. Kufuatia tangazo hilo, mamilioni ya Waislamu duniani kote sasa wanajua rasmi ni lini Eid itasherehekewa mwaka huu.

Katika mataifa haya ya Ghuba, imeelezwa kuwa Eid El-Fitri itasherehekewa siku ya Ijumaa, Machi 20, 2026, baada ya kamati za kuandama mwezi kuthibitisha kuwa mwezi haukuonekana mapema, hivyo Ramadhani kukamilika kwa siku 30.

Kwa ujumla, Waislamu duniani kote wanatarajia kusherehekea siku ya Eid kuanzia kesho na baadhi ya nchi keshokutwa, ingawa mara nyingi hutokea utofauti wa tarehe kutokana na tofauti za uandamaji wa mwezi na maamuzi ya mamlaka za Kiislamu katika nchi husika.

Kwa upande wa Afrika Mashariki, Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) lilitangaza kuwa Eid inaweza kuwa Ijumaa au Jumamosi kutegemea kuandama kwa mwezi. Kuanzia Alhamisi, Machi 19, Waislamu wanaanza kuufuatilia mwezi; ukiandama basi Ijumaa itakuwa Eid, na usipoonekana basi itakuwa Jumamosi. Hali hii pia inafanana na nchi kama Kenya, Uganda, Somalia na Sudan ambapo baadhi ya Waislamu wamefunga siku 29 na wengine 30.

Mambo 10 anayopaswa kufanya Muislam siku ya Eid

1. Kula kabla ya Swala ya Eid Ni Sunna kwa Muislam kuanza siku ya Eid kwa kula kitu kidogo kabla ya kuelekea msikitini kwa ajili ya Swala ya Eid. 2.

 Kumshukuru Mwenyezi Mungu Siku ya Eid ni ya shukrani, hivyo ni muhimu kumshukuru Mungu kwa kukuwezesha kufunga Ramadhani na kufanya ibada.

 3. Kulipa Zakatul-Fitr Kabla ya Swala ya Eid, Muislam anapaswa kuhakikisha ametoa Zakatul-Fitr kwa ajili ya kuwasaidia wenye uhitaji.

 4. Kuoga na kujipamba Usafi ni muhimu siku ya Eid. Inashauriwa kuoga, kuvaa nguo safi au mpya na kujipaka manukato (hasa kwa wanaume). 

 5. Kwenda msikitini na familia Ni vyema kwenda kuswali pamoja na familia, wakiwemo watoto, wanawake na wanaume. 

 6. Kusoma Takbira Takbira ni sehemu muhimu ya siku ya Eid, zikianza tangu usiku wa Eid hadi pale Swala itakapoanza.

 7. Kusikiliza khutba ya Eid Baada ya Swala, ni muhimu kubaki na kusikiliza khutba ya Sheikh kwa ajili ya mawaidha.

 8. Kubadilisha njia ya kwenda na kurudi msikitini Ni Sunna kwa Muislam kutumia njia tofauti anaporudi kutoka msikitini ili kuonesha furaha ya Eid kwa jamii.

 9. Kusherehekea na ndugu na marafiki Baada ya ibada, Waislamu hukutana na ndugu, marafiki na majirani kusherehekea pamoja.

 10. Kutoa sadaka na kusaidia wahitaji Eid ni siku ya kugawana furaha, hivyo ni muhimu kuwasaidia wenye uhitaji ili nao washiriki kikamilifu katika sherehe.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

IRAN YAMTANGAZA AYATOLLAH MPYA

MBUNGE DKT. MAJULE ATOA MSAADA WA VYAKULA, VYANDARUA 100 SHULE YA VIZIWI DODOMA

KWA KHERI MAKARANGA UMEUTIMIZA MWENDO...

Kizza Besigye ‘akamatwa’ tena Uganda

Wasifu wa Kizza Besigye

KWA NINI MAASKOFU JANA KWENYE IBADA YA KUMUAGA PENGO WALIVAA MAVAZI MEUPE WAKATI NI MSIBA..?

KATI YA WATOTO 7 WA HAYATI MAGUFULI ANAYEJULIKANA ZAIDI NI JESCA

WANAOTAZAMWA KUMRITHI AYATOLLAH ALLY KHAMENEI.

MATUKIO RAIS, AMIRI JESHI MKUU DKT. SAMIA AKIZINDUA MAKAO MAKUU YA ULINZI WA TAIFA (MMUT)