Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Iringa, Mhandisi Fatma Rembo, Machi 8, 2026, ameadhimisha Siku ya Wanawake Duniani kwa kufanya matendo ya huruma . Aidha Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi Tanzania (UWT) Taifa, Suzan Peter Kunambi (MNEC) alishiriki katika shughuli hii iliyoandaliwa na Mbunge.
Walitembelea Wodi ya Mama na Mtoto katika Hospitali ya Mkoa wa Iringa pamoja na vituo vya watoto yatima, ikiwemo Kituo cha Faraja kilichopo Kata ya Nduli na Kituo cha Dar-Bilaal-Dar-Fatma kilichopo Kata ya Ilala, ambapo walikabidhi mahitaji mbalimbali kama sehemu ya kuonesha upendo na mshikamano kwa wahitaji hao.












Comments