HONGERA WANAWAKE WOTE – SIKU YA WANAWAKE DUNIANI 🌍


Leo tunapoadhimisha Siku ya Wanawake Duniani, napenda kutoa pongezi za dhati kwa wanawake wote kwa mchango mkubwa wanaoutoa katika familia, jamii na taifa kwa ujumla. 🌸

Mwanamke ni nguzo muhimu ya maendeleo. Kuanzia katika familia, mwanamke ndiye mlezi, mwalimu wa maadili na mjenzi wa msingi wa upendo, amani na mshikamano. Malezi bora ya watoto na vijana yanaanza mikononi mwa mama. đź‘©‍đź‘§‍👦

Katika jamii na taifa, wanawake wana jukumu la kushiriki kikamilifu katika shughuli za maendeleo, kulinda maadili, kuhimiza umoja na amani, na kuwa sauti ya haki na maendeleo kwa wote. 🤝

Ni muhimu tukumbuke kuwa nguvu ya mwanamke si tu katika uwezo wake wa kufanya kazi, bali pia katika hekima yake ya kuunganisha familia, jamii na taifa.

Naomba wanawake wote tuendelee kusimama imara katika wajibu wetu:
✔ Kulea familia zenye maadili
✔ Kuimarisha umoja na amani katika jamii
✔ Kushiriki katika maendeleo ya kiuchumi
✔ Kulinda mustakabali wa taifa letu

Mwanamke akisimama imara, familia inasimama. Familia ikisimama, taifa linakuwa imara.

Hongera sana wanawake wote. Tuendelee kung’ara na kujenga Tanzania yenye amani, upendo na maendeleo. 🇹🇿✨

Happy International Women’s Day!

— Sophia Mwakagenda



 

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

Wasifu wa Kizza Besigye

Kizza Besigye ‘akamatwa’ tena Uganda

IRAN YAMTANGAZA AYATOLLAH MPYA

KILA MWANAMKE ANAPASWA KUFAHAMU HII...

MBUNGE DKT. MAJULE ATOA MSAADA WA VYAKULA, VYANDARUA 100 SHULE YA VIZIWI DODOMA

MAMBO MADOGO YANAYOVUTIA KWA MPENZI WAKO

DKT. MAJULE AKABIDHIWA CHETI CHA SHUKRANI UWT DODOMA KUFANIKISHA USHINDI WA CCM 2025

KWA NINI MAASKOFU JANA KWENYE IBADA YA KUMUAGA PENGO WALIVAA MAVAZI MEUPE WAKATI NI MSIBA..?

WANAOTAZAMWA KUMRITHI AYATOLLAH ALLY KHAMENEI.