MBUNGE DKT. MECKTRIDIS ATOA FEDHA KUWEKA MFUMO WA MAJI KITUO CHA AFYA ITETE ‎

 Mbunge wa Jimbo la Malinyi Mhe. Dkt. Mecktridis Mdaku ametoa msaada wa kuboresha mfumo wa usambazaji majisafi katika kituo cha Afya cha Kata ya Itete, Kilichopo Wilaya ya Malinyi, Mkoani Morogoro na kusaidia kuondoa adha ya upatikanaji wa maji iliyodumu kwa muda mrefu Kituoni hapo.


‎Hatua hiyo imekuja baada ya kuwepo kwa changamoto hiyo kwa muda mrefu iliyoathiri utoaji wa matibabu kwa wagonjwa na wahudumu kushindwa kuhudumia vizuri.


‎Akizungumza wakati wa kukagua ukamilishwaji wa kazi ya kurekebisha mfumo wa maji katika kituo hicho, Mhe. Mbunge Mecktridis amesema kuwa kituo hiki cha afya kinafanya kazi kubwa ya kutoa huduma ya matibabu kwa wagonjwa walio wengi wa Kata hii ya Itete, hivyo ukosefu wa maji katika Kituo hiki ni changamoto inyotishia na inayoathiri shughuli nzima za uuguzi kwa wagonjwa wanaokuja katika Kituo hiki.


‎"Hivyo, tumeona ni vyema kabisa kuweka mfumo huu wa upatikanaji mzuri wa huduma ya majisafi kwa lengo la kuwezesha utoaji mzuri wa huduma mahali hapa," amesema Mhe. Mecktridis.


‎Ameongeza kwa kumpongeza Mhe. Diwani wa Kata ya Itete Dr...Saulo kwa kuibua changamoto hii ya ukosefu wa maji katika kituo chicho na kuifikisha katika ofisi ya Mbunge kwa ajili ya kutafutiwa ufumbuzi wa changamoto hii iliyodumu kwa muda mrefu.


‎Kwa upande wake Daktari Kiongozi wa Kituo cha Afya Itete Dkt. Yusuf Nesta Mgeta amemshukuru Mhe. Mbunge kwa mchango wake wa thamani kwetu kwa kukikumbuka kituo hiki na kusaidia katika kuboresha mazingira ya utoaji tiba kwa wagonjwa.


‎"Kwa sasa maji katika kituo chetu yapo ya kutosha na huduma zinatolewa vizuri kabisa, tunamshukuru sana Mhe. Mbunge," ameeleza Dkt. Yusuf.


‎Naye Bi Janeth Godson mwananchi wa Itete ameishukuru ofisi ya Mbunge kwa kufanya jambo kubwa na la maana kwa kuweka maji katika kituo hicho na kusaidia sana kuboresha huduma nyingi.







 

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

Kizza Besigye ‘akamatwa’ tena Uganda

IRAN YAMTANGAZA AYATOLLAH MPYA

Wasifu wa Kizza Besigye

MBUNGE DKT. MAJULE ATOA MSAADA WA VYAKULA, VYANDARUA 100 SHULE YA VIZIWI DODOMA

KILA MWANAMKE ANAPASWA KUFAHAMU HII...

KWA KHERI MAKARANGA UMEUTIMIZA MWENDO...

KWA NINI MAASKOFU JANA KWENYE IBADA YA KUMUAGA PENGO WALIVAA MAVAZI MEUPE WAKATI NI MSIBA..?

DKT. MAJULE AKABIDHIWA CHETI CHA SHUKRANI UWT DODOMA KUFANIKISHA USHINDI WA CCM 2025

WANAOTAZAMWA KUMRITHI AYATOLLAH ALLY KHAMENEI.