🔴T A N Z I A
Profesa wa Sheria , Mwanafalsafa na Mwanadiplomasia Maarufu, Profesa Costa Ricky Mahalu amefariki Dunia leo Machi 9, 2026 katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete jijini Dar es Salaam akiwa na umri wa miaka 77.
Profesa Mahalu ambaye alizaliwa Julai 9, 1948, katika Kijiji cha Katunguru, wilayani Sengerema, Mkoa wa Mwanza alikuwa msomi mahiri, mwalimu mchapaji kazi, na mwanadiplomasia mwenye uzoefu, aliyesaidia Tanzania kukuza elimu ya sheria na kuimarisha uwakilishi wake kimataifa.

Comments