Shirikisho la Soka la Senegal (FSF) limethibitisha kupokea uamuzi uliotolewa na Kamati ya Rufaa ya CAF kuhusu kupokwa ubingwa wa Kombe la Mataifa la Afrika 2025
FSF imepinga rasmi uamuzi huo ambao wanaona hauna msingi wa kisheria, upo kiholela na hauna uwiano.
FSF inaamini kuna Ukiukaji mkubwa wa kanuni za kifungu cha 82 na 84 cha kanuni za CAF zilizohalalisha maamuzi hayo
FSF imeeleza kuwa mwamuzi wa mechi hiyo alitumia uamuzi wake wa kuchagua kusimamisha mechi kwa muda na sio kusitisha kabisa. Mchezo ulianza tena, penati ilipigwa, na matokeo ya haki yalipatikana
Lakini pia wanaamini Utekelezaji wa kifungu cha 84 ni dhuluma. Wachezaji wa Senegal walirejea uwanjani na mwamuzi alithibitisha hilo, mechi ikaendelea hivyo kifungu cha 84 hakiwezi kufanya kazi
FSF imewaandikia barua CAF ikitaka wasimamishe utekelezaji wa uamuzi huu na kusitisha taratibu zote za kutoa kombe kwa Morocco ikisubiri usuluhishi wa mwisho lakini pia imeeleza nia yake ya kwenda kwenye Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo (CAS) ndani ya saa 48 zijazo ili kutengua uamuzi huu.
Kwenye barua hiyo FSF imeomba kupata ripoti ya waamuzi na maafisa wa mechi hiyo ndani ya masaa 24, isipopata itafungua kesi ya dharula CAS. {Via @officialfelixtz }.

Comments