Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania imeweka wazi kuwa itaendelea kushirikiana na Austria katika
kuimarisha mahusiano ya kidiplomasia yanayolenga kuleta tija ya kiuchumi
na usalama wa jamii.
Hayo yameelezwa Machi 23, 2026, jijini Dar es Salaam wakati wa mazungumzo kati ya Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Mhe. Ayoub Mahmoud (Mb), na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Austria anayeshughulikia masuala ya kisiasa, Mhe. Balozi Dkt. Hannah Liko.
Mazungumzo hayo yalijikita katika kuainisha vipaumbele vya Tanzania ndani ya Mkakati mpya wa Austria kwa Afrika (2026–2029), mkakati ambao unasisitiza ushirikiano wa usawa, ulinzi wa haki za binadamu, na utawala wa sheria kama nguzo kuu za kuelekea maendeleo endelevu.
Kuelekea utekelezaji wa mkakati huo, Mhe. Mahmoud amewasilisha vipaumbele vya Wizara vinavyolenga kuimarisha usalama na uwezo wa kukabiliana na majanga, huku mkazo mkubwa ukiwekwa katika kupambana na uhamiaji haramu, biashara haramu ya binadamu, matumizi ya dawa za kulevya, pamoja na kuzuia uhalifu wa kimtandao ambao umekuwa tishio la kimataifa.
Mhe. Mahmoud amezungumzia mfumo wa Triple-Win, unaolenga kudhibiti uhamiaji haramu huku ukifungua milango ya kisheria kwa vijana wa Kitanzania wenye ujuzi kupata ajira na mafunzo ya ufundi stadi nchini Austria, hatua inayotarajiwa kuwa suluhisho la kudumu katika kuwapatia vijana fursa za kimataifa na kupunguza utegemezi.
Aidha, Tanzania imekaribisha nia ya Austria kuwekeza katika miradi ya nishati safi na uchumi wa kijani kupitia makampuni yake, ili kusaidia mapambano dhidi ya mabadiliko ya tabianchi kupitia miradi ya pamoja ya kitafiti na kiteknolojia.
Kwa upande wake, Dkt. Liko amethibitisha utayari wa Austria kuunga mkono operesheni za kikanda za kulinda amani za Umoja wa Mataifa na kuongeza kuwa Austria itaendelea kuwa mshirika wa kimkakati katika kukuza viwanda, sayansi, na utamaduni ili kuhakikisha Tanzania inabaki kuwa mazingira salama kwa raia, uwekezaji, na utalii kwa manufaa ya mataifa yote mawili.
Vilevile amesema kupitia Shirika la Maendeleo la Austria (ADA), nchi hiyo imeahidi kuendelea kuwa mshirika wa kimkakati wa Tanzania katika kukuza utamaduni, sayansi, na maendeleo ya kijamii.

Comments