UWT KIBAHA YAWAHIMIZA WANAWAKE KUANZISHA VIKUNDI VYA UJASIRIAMALI

NA VICTOR MASANGU,KIBAHA

 Uongozi wa Jumuiya ya umoja wa wanawake (UWT)  Wilaya  ya  Kibaha  mjini umewahimiza wanawake kuhakikisha kwamba wanajiunga kwa pamoja katika  kujiunga na vikundi mbali mbali vya ujasiriamali  ikiwemo kutumia fursa za kuchukua mikopo ambayo itaweza kuwasaidia kwa kiasi  kikubwa katika kujikwamua kiuchumi na kuondokakana na wimbi la umasikini.


Kauli hiyo imetolewa na  Mwenyekiti wa (UWT) Wilaya ya Kibaha Elina Mgonja wakati wa ziara maalumu yenye lengo la kuweza kuwashukuru wanawake kwa kuweza  kushirikiana bega kwa bega  katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 na kupelekea chama cha mapinduzi (CCM)7 kuweza kushinda kwa kishindo katika viti vitatu vya Udiwani, Ubunge pamoja na nafasi ya Urais.

Mwenyekiti huyo ameweza kufanya ziara hiyo maaalumu katika kata mbili za Maili moja na Kata ya Tangini ambapo ameongozana na baaadhi ya wajumbe wa kamati ya utekelezaji kwa lengo la kuweza kuzungumza na wanawake hao  kusikiliza baadhi ya chanagmoto zao pamoja na kuwashukuru kwa  kukipigia kura nyingi za kishindo  chama cha mapinduzi (CCM) na kufanikiwa kuwapata viongozi wa nafasi mbali mbali.

"Tumeanza ziara yetu tangu tarehe  10  mwezi huu na lengo letu kubwa ni kutembelea katiika kata zote 14 kwa ajili ya kukutana na  wanawake ikiwa ni kutoa shukrani za dhati nikiwa pamoja na katibu  wangu wa UWT  ambapo tumeongozana kwa pamoja na baadhi ya wajumbe wwa kamati ya utekelezaji ambapo kwa leo tumefanya ziara katika kata ya Mail moja na pamoja na Tangini.

Pia Mwenyekiti huyo amebainisha kwmaba lengo lingine la ziara hiyo ya kuweza kuimarisha jumuiya hiyo kuanzia ngazi za matawi na kuwataka viongozi mbali mbali wa matawi kuhhakikisha wanavunja makundi na kuungana kwa pamoja kwani uchaguzi mkuu umeshamalizika hivyo kitu kikubwa ni kuwa na umoja na mshikamano.

Kadhalika Mwenyekiti huyo amempongeza kwa dhati Rais wa awamu ya sita kwa kuweza kutekeleza ilani ya cchama kwa vitendo ikiwemo kutenga fedha nyingi ambazo zimekwenda kutekeleza miradi mbali mbali ya maendeleo ikiwemo sekta ya afya, eilimu, maji, nishati ya umeme pamoja na huduma za kijamii.

Kwa upande wake Katibu wa UWT Wilaya ya Kibaha Cesilia Ndalu amebainisha kwamba  ziara hiyo pia imelenga kuanzisha vikundi vya uchumi ambavyo vitaweza kuwasaidia kwa kiasi kukubwa kupambana na wimbii la umasikini.
 
Diwani wa kata ya Mail moja Ramadhani Lutambi ameahidi kuzishughulikia  changamoto mbali mbali walizonazo wanwawake ikiwemo suala la kuweza kuwasimamia kujiungha katika vikundi mbali mbali vya ujasiriamali pamoja na kuwapambania kuweza kupata fursa za mikopo ambayo itawasaidia katika kujikwamua kiuchumi.

Ziara ya jumuiya ya wanawake Wilaya ya Kibaha mjini ambayo ilianza rasmi  tangu Machi kumi mwaka huu imeweza kuleta mafanikio makubwa naakupokelewa na wanawake kutoka kata mbali mbali amnbao wameweza kutoa pongezi  zao za dhati kwa ziara hiyo ya  uongozi wa UWT ambayo  imeweza kuleta matumaini makubwa baada ya kumalizika kwa uchaguzi mkuu.






 

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

IRAN YAMTANGAZA AYATOLLAH MPYA

MBUNGE DKT. MAJULE ATOA MSAADA WA VYAKULA, VYANDARUA 100 SHULE YA VIZIWI DODOMA

Kizza Besigye ‘akamatwa’ tena Uganda

Wasifu wa Kizza Besigye

KWA KHERI MAKARANGA UMEUTIMIZA MWENDO...

KWA NINI MAASKOFU JANA KWENYE IBADA YA KUMUAGA PENGO WALIVAA MAVAZI MEUPE WAKATI NI MSIBA..?

WANAOTAZAMWA KUMRITHI AYATOLLAH ALLY KHAMENEI.

MATUKIO RAIS, AMIRI JESHI MKUU DKT. SAMIA AKIZINDUA MAKAO MAKUU YA ULINZI WA TAIFA (MMUT)

KIJANA WA KINYAKYUSA WA ENZI HIZO, NUSURA AMCHAPE WAZIRI MUONGO BUNGENI