VYAKULA MAARUFU ZAIDI WAKATI WA DAKU NA KUFUNGA AFRIKA

Pilau ya nyama ni chakula maarufu nchini Kenya.
Muda wa kusoma: Dakika 2

Wakati wa mfungo wa mwezi wa Ramadhani, kuna ongezeko la hamu ya kula vyakula mbalimbali.

Wengine hufikiria manufaa ya afya na mazingira wanapochagua kile wanachokula kwa kiamsha-kiamsha kinywa au chakula cha kufungua .

Wakati familia zikitafakari asili ya mfungo wao wa Ramadhani na mlo wa kabla ya alfajiri, tulizungumza na baadhi ya wawakilishi wetu kutoka nchi za Afrika ili kujua ni vyakula gani huliwa sana katika nchi zao kwa ajili ya milo ya kabla ya alfajiri na mfungo wa Ramadhani.

Morocco

"Wakati wa kufuturu, tunaanza na tende na maziwa. Kisha tunakula kile tunachokiita harira - aina ya uji ambao ni kama supu na ni mtamu, unaotia nguvu na kupasha joto tumbo," anasema mwandishi wa BBC Basma El Atti.

Wakati wa sahur, "mara nyingi tunakula kitu kinachoitwa Sellou - kipande cha mkate na karanga, na kisha tunakunywa maji mengi."

Tanzania

Nchini Tanzania waumini hula Mihogo ya nazi, viazi vitamu, samaki, nyama na tambi. Mara nyengine hula magimbi, maharage na vitu vya ngano kama maandazi na chapati

Nigeria



Supu ya Tuwo na egusi, ni aina ya mlo mzito unaotolewa kwa sauhur nchini Nigeria

Ahmed Ambali kutoka Nigeria anasema, "Wakati wa mfungo, tunapendelea kula chakula chepesi. Tunakula kwa nguvu na shauku nyingi. Chakula chepesi ni bora baada ya tumbo tupu kwa muda mrefu."

Vipi kuhusu sahur?

Senegal

Wali uliopikwa ni chakula maarufu zaidi cha kiamsha kinywa nchini Senegal.

Watu wa Senegal "Wakati wa mfungo, tunakunywa chai ya mitishamba iliyo na viungo vya dawa na tende.

Huu ni mchanganyiko ambao utasaidia kusafisha tumbo," alisema Khadidiatou Cisse.

Aliongeza, "Kwa sahur, kila mtu hula vitu tofauti, haswa wali uliopikwa, lakini tunatumia supu ya mboga."

Kenya



Mlo wa Samosa na Bhajia

"Tunakula samosa, bhajia na chapati kabla ya kula mlo mzito kama pilau," anasema Nasteha Mohammed.

Kwa suhur, "tunapendelea kula kitu chepesi kama chai, mtindi, chapati, na chakula chochote ambacho kinaweza kudumisha mwili wako kwa siku, hata wakati wa joto la mchana."


 

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

Wasifu wa Kizza Besigye

Kizza Besigye ‘akamatwa’ tena Uganda

IRAN YAMTANGAZA AYATOLLAH MPYA

KILA MWANAMKE ANAPASWA KUFAHAMU HII...

MBUNGE DKT. MAJULE ATOA MSAADA WA VYAKULA, VYANDARUA 100 SHULE YA VIZIWI DODOMA

MAMBO MADOGO YANAYOVUTIA KWA MPENZI WAKO

DKT. MAJULE AKABIDHIWA CHETI CHA SHUKRANI UWT DODOMA KUFANIKISHA USHINDI WA CCM 2025

KWA NINI MAASKOFU JANA KWENYE IBADA YA KUMUAGA PENGO WALIVAA MAVAZI MEUPE WAKATI NI MSIBA..?

WANAOTAZAMWA KUMRITHI AYATOLLAH ALLY KHAMENEI.