WATANZANIA SABA WAWASILI NCHINI KUTOKEA IRAN

 Watanzania SABA waliokuwa nchini Iran wamewasili jijini Dar es Salaam Machi 13, 2026, kufuatia operesheni ya uokozi iliyoratibiwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Watanzania hao wamewasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) saa 8:40 usiku kwa kutumia Shirika la Ndege la Uturuki, wakitokea nchini Uturuki ambako walipokewa awali baada ya kuvuka mpaka wa nchi kavu wakitokea nchini Iran.

Katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNIA) Watanzania hao walipokelewa na Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Abdallah Kilima na maafisa wengine wa Wizara.

Mapokezi ya Watanzania hao yaligubikwa na hisia za faraja kutoka kwa ndugu na jamaa waliokuwa na hofu kubwa juu ya hatima ya usalama wa wapendwa wao.

Wakizungumza baada ya kuwasili uwanjani hapo Watanzania hao wameishukuru Serikali kwa kuratibu suala la kurejeshwa kwak nchini kwani imekuwa ni faraja kubwa kwao kurudi nyumbani salama kutokana na machafuko yanayoendelea nchini iran.

Serikali ya Tanzania ilichukua hatua za dharura kulinda maisha ya raia wake waliokuwa nchini humo kwa masomo na shughuli nyingine.

Safari ya kurejea nyumbani kwa Watanzania hao ilianzia kwenye mpaka wa Razi (Iran) na kufika Kapıkule (Uturuki) mnamo Machi 11, 2026 na kupokelewa na Balozi wa Tanzania Uturuki Mheshimiwa Iddi Seif Bakari na maafisa wa Ubalozi wa Tanzania nchini humo.

Serikali ya Tanzania ilichukua hatua za dharura kuokoa maisha ya raia wake waliokuwa nchini Iran kwa masomo na shughuli nyingine.

Watanzania hao waliorejea nyumbani wana hali nzuri kiafya na Serikali itaendelea kufuatilia kwa karibu hali ya usalama katika ukanda wa nchi za Ghuba ili kuhakikisha Watanzania wengine waliosalia katika nchi hizo wanakuwa salama.





Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

Kizza Besigye ‘akamatwa’ tena Uganda

IRAN YAMTANGAZA AYATOLLAH MPYA

Wasifu wa Kizza Besigye

MBUNGE DKT. MAJULE ATOA MSAADA WA VYAKULA, VYANDARUA 100 SHULE YA VIZIWI DODOMA

KILA MWANAMKE ANAPASWA KUFAHAMU HII...

KWA KHERI MAKARANGA UMEUTIMIZA MWENDO...

KWA NINI MAASKOFU JANA KWENYE IBADA YA KUMUAGA PENGO WALIVAA MAVAZI MEUPE WAKATI NI MSIBA..?

DKT. MAJULE AKABIDHIWA CHETI CHA SHUKRANI UWT DODOMA KUFANIKISHA USHINDI WA CCM 2025

WANAOTAZAMWA KUMRITHI AYATOLLAH ALLY KHAMENEI.