Wakala wa Vipimo (WMA) wameshiriki katika maadhimisho ya Siku ya Wanawake Kimataifa, kwa kutoa elimu ya vipimo kwa wadau mbalimbali waliofika Kongwa, Dodoma mahali ambako sikukuu hiyo imefanyika ngazi ya Mkoa.
Akieleza kuhusu huduma zilizotolewa katika maonesho hayo, Meneja Mawasiliano wa WMA, Veronica Simba amesema ni pamoja na elimu kuhusu uandishi wa alama sahihi za vipimo katika bidhaa pamoja na kuhamasisha matumizi ya vipimo sahihi na kwa usahihi.
"Mahala hapa tumekutana na wanawake wengi ambao ni wajasiriamali na tumefanikiwa kuwapatia elimu ya matumizi sahihi ya vipimo kwa ajili ya biashara zao hivyo tumefanikiwa kama tulivyotarajia," amesema.
Vilevile, Simba ameongeza kuwa wamefanikiwa kutoa elimu ya vipimo kwa makundi mengine mbalimbali ya wanawake, wakiwemo watumishi wa umma, wawekezaji na hata kina mama wa nyumbani.
Amesema kuwa, makundi yote hayo yanahitaji elimu kuhusu umuhimu wa matumizi sahihi ya vipimo ili kila mmoja anufaike kulingana na uhitaji wake.







Comments