Waziri wa Mambo ya Ndani nchini Tanzania, George Simbachawene amewashukuru Watanzania kwa kuonesha utulivu na uzalendo katika kuilinda amani ya taifa, hususan katika kipindi hiki ambacho Tanzania inaadhimisha miaka 64 ya Uhuru wa Tanganyika. Akizungumza Jumanne, Desemba 9, 2025 jijini Dar es Salaam wakati wa ukaguzi wa hali ya ulinzi na usalama kwenye mitaa mbalimbali, Waziri Simbachawene ameelekeza wananchi kuendelea na shughuli zao kama kawaida leo Jumatano, Desemba 10, 2025. Amesema vyombo vya ulinzi na usalama vinaendelea kuimarisha ulinzi katika maeneo mbalimbali nchini ili kudumisha amani na utulivu, na kusisitiza kuwa serikali inaamini katika mazungumzo, utulivu na kustawisha maendeleo ya nchi. Wananchi pia wameonesha kuridhika na hatua za ulinzi zinazochukuliwa, wakisisitiza umuhimu wa kudumisha amani kwa faida ya kila Mtanzania.
- Get link
- X
- Other Apps