IKULU YALIKANA GARI LILILOKAMATWA NA CHADEMA ARUSHA

UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

Telephone: 255-22-2114512, 2116539

Fax: 255-22-2113425


PRESIDENT’S OFFICE,
      THE STATE HOUSE,
       P.O. BOX 9120,  
DAR ES SALAAM.
Tanzania.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Mapema wiki hii, kumetolewa na kunukuliwa taarifa zinazodai kuwa gari la Ikulu lilikamatwa na wafuasi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), huko Arusha.
Ikulu imefanya utafiti na ukaguzi katika idara zake zote na kubaini kuwa taarifa hizo sio za kweli na ni za kusadikika tu kutoka kwa watu waliokuwa na hisia zao potofu.
Taarifa hizo zilizotolewa na kusambazwa kwenye vyombo mbalimbali, zimedai kuwa gari hiyo, yenye namba za usajili T 856 ACY aina ya Toyota Land Cruiser VX, ambalo halikuwa na nyaraka muhimu kwa ajili ya usalama pia lilikuwa na namba TZS 4930 katika vioo vyake,
Napenda kusisitiza na kudhibitisha kuwa gari hiyo siyo ya Ikulu na wala katika idara zake zingine hakuna gari yenye usajili wala namba hizo.
Napenda kuwashauri waandishi kuwa makini na kufuata weledi zaidi kwa kuhakikisha na kutafuta ukweli wa habari wanazotoa na kuandika wakati wote na hasa katika kipindi hiki muhimu cha kuelekea kwenye uchaguzi mkuu, kwani weledi na usahihi wa habari ndiyo utaweka historia na kutunza heshima ya taaluma yenu.
Imetolewa na Premi KIbanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais, Msaidizi
Ikulu
DAR ES SALAAM.
22 Oktoba, 2010

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

KANUNI 10 ZA MAHUSIANO YENYE FURAHA

HAKI 13 ZA MWANAMKE LAZIMA MWANAUME AZIHESHIMU:

MAMBO SABA AMBAYO WANAUME WENGI HAWAYAPENDI:

NI HESHIMA KUBWA SANA KUIFUNDISHA YANGA - KOCHA MPYA WA YANGA

RAIS DKT.MWINYI: ZANZIBAR KUWA KITUO CHA BIASHARA CHA KIMATAIFA

”RAIS SAMIA AUMIZWA MAUAJI YA KIBIKI”

KOCHA SEAD RAMOVIC AMRITHI GAMONDI YANGA.

UOKOAJI KARIAKOO NI USHUHUDA WA MOYO WA UTANZANIA: NCHIMBI

ACHENI KUWA CHANZO CHA CHOKOCHOKO NA VURUGU - ASKOFU CHANDE