Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji wa Baraza Kuu la Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Ridhiwani Kikwete (kulia) akilakiwa kwa furaha na Mwenyekiti wa zamani wa umoja huo, ambaye ni Mgombea ubunge wa Jimbo la Kikwajuni Zanzibar kupitia CCM,Hamad Masauni Yusufu alipowasili kumpa nguvu katika kampeni mjini Unguja juzi. (PICHA NA RICHARD MWAIKENDA) |
WAZIRI BASHE APIGA MARUFUKU WASIOSOMEA KILIMO KUUZA PEMBEJEO
WAZIRI wa Kilimo, Hussein Bashe amepiga marufuku wasiosomea masuala ya Kilimo kuuza pembejeo. Amesema kuwa masharti ya muuza pembejeo lazima awe amesomea Kilimo kwa ngazi ya cheti, diploma na Digrii. Ameyasema hayo alipokuwa anazungumza na wadau wa mbegu katika mkutano uliofanyika jijini Dodoma. "Haiwezekani wanaowashauri na kuwauzia mbegu wakulima wasiwe na utalaamu wa sekta hiyo, mbona wanaogawa dawa na kutibu wagonjwa wamesomea ufamasia, uuguzi na udaktari, kwa nini isiwe kwenye Kilimo? Amehoji Waziri Bashe. Amewapa kipindi cha mpito cha mwaka mmoja wauzaji kwenda kusomea Kilimo ili waruhusiwe kisheria kuuza Pembejeo na kwamba baada ya hapo sheria itafuata mkondo wake kwa kukagua maduka yote ya pembejeo na kuwakamata watakaobainika.
Comments