WATU wanne wamenusurika kufa katika ajali hiyo Jijini Mbeya baada ya ndege waliyokuwa wakisafiria kuanguka muda mfupi baada ya kuruka kutoka uwanja wa ndege wa Mbeya katika eneo la Uyole nje kidogo ya Jiji waliokuwepo katika ndege hiyo ni pamoja na Rubani wa ndege hiyo, Justin Verman ambaye ni raia wa Afrika ya kusini alisema kuwa ajali hiyo ilisababishwa na hitilafu iliyokuwepo kwenye injini hali iliyosababisha ikose mwelekeo.
Verman aliwataja waliokuwemo katika ndege hiyo kuwa ni Meneja wa Shamba la Kapunga Sunil Tahil (50),Meneja Utawala Christian basil(30) raia wa Tanzania pamoja na Mohamed Mmasi ambaye ni Meneja wa usafirishaji wa Kampuni hiyo ya ETC-BIO Energy.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoani,mbeya Anacletus Malindisa amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na hakuna mtu yeyote aliyejeruhiwa kutokana na ajali hiyo na kwamba uchunguzi unaendelea.
Comments