NEW YORK, Marekani
VIDEO iliyoonyweshwa mwishoni mwa wiki katika mitandao mbalimbali ya kijamii, ambayo ilielezea madhara ya taratibu anayoyapata mwanamke aliyeongeza ukubwa wa makalio, kwa dawa za silkoni imewashtua wanawake wengi waliowahi kutumia aina yoyote ya madawa hayo.

Taarifa hiyo ilieleza kuwa madawa hayo badala ya
kumfanya mwanamke awe laini, video hiyo inaelezea namna ukuaji wa haraka
wa makalio pamoja na kuathirika huku yakiachwa katika sura mbaya sehemu
za nyuma (chini) baada ya muda mfupi.
Imebainika kuwa pamoja na dawa za kuongeza ukubwa
wa makalio ya akina dada kupendwa, dawa hizo pia zina madhara kwa afya
ya binadamu.
Wataalamu wa mambo wanadai kwamba pamoja na
kuongeza ukubwa wa makalio pia dawa huleta matatizo ya kuvimba kwa ngozi
ya makalio katika mpangilio usio sahihi.
Dawa hizo pia zimetajwa kuwa husababisha kwa uwepo mkubwa wa ugonjwa wa saratani.
Video hiyo ya sekunde 20, inamwonyesha mwanamke aliyeongeza makalio yake kwa dawa za silicone akionyesha namna alivyoathirika kutokana na matumizi ya madawa hayo huku akisema : "Hivi ndivyo nilivyoongeza ukubwa wa makalio yangu".

Anaongeza: "Sidhani kama ni sahihi kufanya hivi.
Nadhani kuna ulazima wa kuyaondoa haya makalio yangu yote kwa sasa."
alisikika akisema.
Mpaka kufikia jana video hiyo ambayo pia iliwekwa
katika mtandao wa kijamii wa Facebook tayari ulikuwa umependezwa na watu
278,000 wanaotembelea huku ikiwa imehamishwa na watu zaidi ya 430,000
wakipeleka katika kurasa zao.
Mtumiaji mmoja wa mtandao huo kutoka nchini
Marekani Donna Wright-Levy, alichangia akisema: "Mimi hupendelea kwenda
maeneo kadhaa ambako hutengenezwa shepu yangu kwa madawa haya sasa nina
ulazima wa kwenda kupima saratani".
Ni vigumu kuthibitisha mwanamke huyu alitumia
kliniki gani wakati alipofanyiwa uongezwaji wa ukubwa wa makalio yake
miaka miwili iliyopita.
Lakini mmoja wa madaktari kutoka kliniki ya
upasuaji ya BAAPS Aurora nchini Uingereza Adrian Richards, ambaye pia ni
mshauri wa upasuaji anaamini kuwa mwanamke huyo alifanyiwa marekebisho
ya makalio yake kwa dawa za silicone.
Alisema tatizo hutokea wakati nyama ya makalio
inaposhindwa kuulinda vema mwili na kuwa imara katika nyama na mifupa na
hivyo madhara huanza kutokea juu ya ngozi na kusambaa mpaka ndani ya
nyama na baadaye mfupa.
Ni matatizo ambayo ni ya kawaida kumfika mtumiaji
ya dawa za kuongeza ukubwa wa maumbile iwe ni matiti ay makalio. Ni
lazima itokee baada ya muda maana kama kitu kilipulizwa na upepo ina
maana wakati wake ukiisha kitarudi kama awali.
"Huyu mwanamke aliyaongeza makalio yake kwa nyuma
na kwa juu zaidi hivyo tayari madhara yake yamekuwa ni makubwa kwa maana
hakufanya upasuaji bali alitumia njia za mkato za silicone, " alisema
Richards.
Comments