SHEREHE ZA KIMASAI ZA VIJANA KUANZA KUNYWA MAZIWA



Mgeni rasmi, Peter Kiroya (wa pili kushoto) mkazi wa Manyara wilayani Simanjiro ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Kakonko, mkoani Kigoma, akiwaongoza vijana wa kimasai kundi la Korianga kuingia kwenye boma kwa ajili ya kushiriki sherehe ya unywaji wa maziwa ikiwa ni mojawapo ya hatua ya makuzi  kwa vijana mkoani Manyara juzi,  Wa pili kulia ni Mke wa mkuu huyo wa wilaya, Filomena Kiroya.


Mkuu wa Wilaya ya Kakonko, mkoani Kigoma, Peter Toima akipokea kibuyu cha maziwa kutoka kwa mkewe, Filomena Kiroya kama ishara ya kuwaonesha vijana waliohitimu hatua moja ya makuzi katika sherehe za unywaji wa maziwa mkoani Manyara katika Wilaya ya Simanjiro.

: Mmoja wa vijana wa kimasai kundi la Korianga akipokea kibuyu cha maziwa kutoka kwa mke wake kama ishara kuwa kuanzia sasa anaruhusiwa kunywa maziwa katika boma lake bila ya kujificha kama alivyokuwa akifanya kabla ya kuingia katika hatua hiyo ya makuzi kwa vijana wa kimasai.


Onesmo Toima akinywa maziwa yaliyomo katika kibuyu baada ya kuvuka hatua ya malezi iitwayo ‘Sporio’ na kuingia hatua ya Korianga katika sherehe za unywaji wa maziwa zilizofanyika jana mkoani Manyara katika Wilaya ya Simanjiro.


: Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Venerose Mtenga akihutubia wakati wa sherehe hizo. Kulia ni mgeni rasmi wa sherehe hiyo, Peter Kiroya ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Kakonko mkoani Kigoma.


Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Venerose Mtenga (aliyekaa kulia) akiwa katika picha ya pamoja na vijana wa kundi la Korianga, Wa tatu kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Kakonko. Peter Kiroya. Wa pili kulia ni Mke wa mkuu huyo wa wilaya, Filomena Kiroya.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

UKWELI KUHUSU TENDO LA NDOA NA FAIDA ZAKE

HUYU NDIYE WANU HAFIDH, CHAMPIONI WA ELIMU

MAWAZIRI WALIOACHWA HAWA HAPA

๐Œ๐‰๐”๐„ ๐Š๐€๐‚๐‡๐„๐‘๐Ž ๐Œ๐™๐„๐๐€

HISTORIA YA MAREHEMU MC PILIPILI

VITU 10 WANAUME WANAVYOPENDA ZAIDI TOKA KWA MWANAMKE — SIYO SURA, SIYO MWILI ❤️

USIKUBALI KUWA LOFA KWA MWANAMKE...

NAPE AWAPA UKWELI VIJANA