Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hassan, amemteua mbunge wa Makunduchi, Wanu Hafidh Ameir kuwa Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia. Swali; Wanu ni nani? Kwa nini yeye nafasi ya Naibu Waziri wa Elimu? Jibu la kwanza ni hili; Wanu ni championi wa elimu. Jibu la pili; Wanu ni shujaa wa nishati safi ya kupikia. Wanu ni mwanasheria msomi. Kijamii ni Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi isiyo ya kiserikali ya Mwanamke Initiatives Foundation (MIF). Taasisi hiyo, imejikita katika kuwajenga na kuboresha maisha ya wanawake, vijana na watoto, kuanzia kwenye afya, elimu na uchumi. Shabaha kubwa ya MIF ni kushughulikia matatizo ya kijamii ndani ya Zanzibar na Tanzania kwa jumla, kupitia utekelezaji wa mikakati ya kiulimwengu. Madhumuni mama ya MIF ni kuzijengea uwezo jamii za Tanzania, kwa kuboresha elimu, kustawisha afya, kuchochea maendeleo ya kiuchumi, ili kuukabili na kuushinda umaskini, ujinga na maradhi, kupitia uongozi na juhudi za pamoja. Jimbo la Makunduchi, Zan...
Comments