Sure Boy, Andabwile ‘watemwa’ Yanga ikiifuata MC Alger BENCHI la Ufundi la Yanga chini ya Kocha Mkuu Sead Ramovic, limetangaza majina ya ‘askari 24 wa Jeshi la Wananchi’ hao wanaokwea pipa leo alasiri ya leo Jumanne Desemba 3, kwenda Algiers, nchini Algeria, kuwavaa Mouloudia Club d’alger ‘MC Alger,’ huku Salum Aboubakar ‘Sure Boy na Aziz Andabwile wakiachwa. Yanga watakuwa wageni wa MC Alger Jumamosi ya Desemba 7, katika mechi ya pili ya Kundi A la Ligi ya Mabingwa Afrika (CAF CL 2024/25), wakiwa na kumbukumbu ya kipigo cha mabao 2-0 kutoka kwa Al Hilal ya Sudan, huku Waalgeria hao wakitoka kugawana pointi na TP Mazembe katika mechi ya kwanza. Kwa mujibu wa uongozi wa Yanga, kikosi chao kinajumuisha wachezaji 24, wakiwemo nyota wao kadhaa waliokuwa majeruhi na waliokuwa wakitumikia adhabu zilizowakosesha mechi ya Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara, waliyoshinda kwa mabao 2-0 dhidi ya Namungo FC ya Ruangwa, Lindi. Katika orodha ya nyota wanaokwea pipa alasiri hii ya leo, Yanga itaongoz...
Comments