MABADILIKO YA TABIANCHI YAZUA MALUMBANO WAKATI WA MAFUNZO TGGA+video

 

 

Wakufunzi wakijadiliana jambo wakati wa mafunzo ya  mabadiliko ya Tabianchi yaliyoandaliwa na TGGA katika Baraza la Maaskofu (TEC), Kurasini jijini Dar es Salaam.

Wakufunzi wa Programu ya Mabadilikio ya Tabianchi Duniani wakilumbana kwa kila upande wa wanasayansi na wasioamini kuhusu mabadiliko ya Tabianchi kuvutia upande wake wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo wakufunzi hao kuhusu namna ya kwenda kutoa elimu kwa jamii jinsi ya kupambana na athari ya mabadiliko hayo.

Mafunzo hayo ya siku tano yanayofanyika katika Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC), yamehudhuriwa na wakufunzi wa Chama cha Skauti wa Kike Tanzania (Tanzania Girl Guides Association,TGGA) kutoka mikoa 12 nchini na wengine kutoka Benin na Lesotho pamoja na wakufunzi wa kujitolea kutoka chama cha Girl Guides Duniani cha WAGGGS.

Meneja wa programu hiyo, David Mbumila mwishoni anaelezea jinsi walivyouandaa mjadala huo lengo likiwa ni kuwajengea uwezo zaidi wa uelewa na namna ya kwenda kutoa elimu sahihi kwa jamii kuhusu mabadiliko hayo.
IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA
 
0754264203

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

MJUE VIZURI KOCHA MPYA WA YANGA PEDRO

RAIS SAMIA SIO RAIS JOYCE BANDA WA MALAWI, TANZANIA SIO KENYA

IJUE HISTORIA YA PACOME ZOUZOUA

BALOZI MIGIRO AKUTANA NA JOPO LA WAANGALIZI WA UCHAGUZI MKUU WA UMOJA WA AFRIKA