MZEE KIKWETE AKABIDHI UJUNBE MAALUMU WA RAIS KWA RAIS WA NIGER


 NIGER — Rais Mstaafu wa Tanzania na Mjumbe Maalum wa Rais Samia Suluhu Hassan, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete, amekutana na Rais wa Niger, Jenerali Abdourahamane Tchiani, katika Ikulu ya Taifa jijini Niamey.


Katika kikao hicho, Kikwete, ambaye ni mwanadiplomasia mwenye uzoefu mkubwa, alikabidhi ujumbe maalum kutoka kwa Rais Samia. Alimfikishia salamu za upendo na pongezi kutoka kwake pamoja na kuonyesha shukrani kwa uhusiano mzuri uliopo kati ya Tanzania na Niger. Aidha, alisisitiza umuhimu wa kuimarisha zaidi ushirikiano huo hususan katika maeneo ya biashara, uwekezaji na utalii.


Vilevile, Kikwete alieleza kuwa kuna haja kwa mataifa ya Afrika kushirikiana katika kubadilishana uzoefu, maarifa na ujuzi ili kuweza kutumia rasilimali nyingi zilizopo barani kwa manufaa ya watu wake.


Imeandaliwa na Mwandishi Wetu


Zaidi tembelea //habarileo.co.tz

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

UKWELI KUHUSU TENDO LA NDOA NA FAIDA ZAKE

HUYU NDIYE WANU HAFIDH, CHAMPIONI WA ELIMU

MAWAZIRI WALIOACHWA HAWA HAPA

๐Œ๐‰๐”๐„ ๐Š๐€๐‚๐‡๐„๐‘๐Ž ๐Œ๐™๐„๐๐€

HISTORIA YA MAREHEMU MC PILIPILI

VITU 10 WANAUME WANAVYOPENDA ZAIDI TOKA KWA MWANAMKE — SIYO SURA, SIYO MWILI ❤️

USIKUBALI KUWA LOFA KWA MWANAMKE...

NAPE AWAPA UKWELI VIJANA