RAIS SAMIA AIPONGEZA SIMBA KUINGIA NUSU FAINALI

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameipongeza Simba SC kwa kufanikiwa kufuzu kwenda nusu fainali ya Kombe la Shirikisho barani Afrika kwa ushindi wa mikwaju ya penalti 4-1.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Rais Samia ameweka ujumbe uliosomeka hivi:

“Pongezi za dhati kwa Klabu ya Simba kwa ushindi katika mchezo wa mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika (CAF Confederation Cup). Ushindi wenu ni furaha kwa mashabiki wenu na burudani kwa Watanzania wote. Ninawatakia kila la kheri katika Nusu Fainali.”

Simba amepata ushindi huo katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam baada ya mchezo wa awali uliopigwa nchini Misri kumalizika kwa Mnyama kufungwa 2-0 naye alipofika kwa Mkapa, akamchinja 2-0 kisha wakaenda kwenye mikwaju ya penalti na safari ya Mwarabu kwenye mashindano hayo ikaishia hapo!




 

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

UKWELI KUHUSU TENDO LA NDOA NA FAIDA ZAKE

HUYU NDIYE WANU HAFIDH, CHAMPIONI WA ELIMU

MAWAZIRI WALIOACHWA HAWA HAPA

๐Œ๐‰๐”๐„ ๐Š๐€๐‚๐‡๐„๐‘๐Ž ๐Œ๐™๐„๐๐€

HISTORIA YA MAREHEMU MC PILIPILI

VITU 10 WANAUME WANAVYOPENDA ZAIDI TOKA KWA MWANAMKE — SIYO SURA, SIYO MWILI ❤️

USIKUBALI KUWA LOFA KWA MWANAMKE...

NAPE AWAPA UKWELI VIJANA