Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe amesema kuwa viwanda viwili vya kuchakata chai kuanzishwa nchini ili kuliokoa zao hilo. Viwanda hivyo vitajengwa wilayani Kilolo mkoani Iringa na Rungwe, Mbeya. Pamoja na mambo mengine ameyasema hayo alipokuwa akihutubia katika mkutano Mkuu wa Wadau wa Tasnia ya zao hilo uliofanyika Aprili 8, 2025 jijini Dodoma.
Aidha, Bashe amesema kuwa serikali iko tayari kuweka miundombinu ya umwagiliaji kwenye mashamba ya chai nchini.
Pia amebainisha kuwa Benki ya Maendeleo ya Ushirika itazinduliwa Aprili 28, 2025 na itakuwa na matawi katika mikoa mbalimbali nchini.
0754264203
Comments