Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Prof. Paramagamba Kabudi amesema lengo la kuanzisha Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari ni kuifanya Taaluma ya uandishi wa habari iheshimike sawa na taaluma za uhandisi, udaktari na uanasheria.
Aidha, amesema kuwa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), litafanyiwa maboresho makubwa ikiwemo usikivu na kuanzishwa wa idha ya nje kwa lugha ya kiingereza.
Pamoja na mambo mengine Prof. Kabudi ameyasema hayo katika Ukumbi wa Idara ya Habari MAELEZO jijini Dodoma Aprili 14, 2025, alipofungua dimba la mawaziri kuzungumza na vyombo vya habari kuhusu kuhusu mafanikio ya wizara katika kipindi cha uongozi wa Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan.Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamadunim Sanaa na Michezo ambaye pia ni Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa akitoa neno la utangulizi alipokuwa akimkaribisha Waziri Kabudi.
Msigwa akiwa na Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari MAELEZO, Rodney Thadeus.
Waandishi wa habari wakiwa katika mkutano huo.
Waziri Kabudi akiwa na wanahabari.Msigwa akiwa na Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari MAELEZO, Rodney Thadeus.
MSIMAMIZI MKUU
KAMANDA WA MATUKIO ONLINE TV
0754264203
Comments