MABINGWA wa Tanzania Bara, Yanga kuingia Nusu Fainali ya Kombe la Mapinduzi, michuano hiyo maalum ya kuazimisha miaka 61 ya Muungano baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya KVZ usiku huu Uwanja wa Gombani, Pemba.
Ilikuwa siku nzuri kwa winga Dennis David Nkane aliyetoa pasi ya bao la kwanza lililofungwa na kiungo Mburkinabe, Stephane Aziz Ki dakika ya 28, kabla ya yeye mwenyewe kufunga la pili dakika ya 86.
Yanga sasa itakutana na Zimamoto iliyoitoa Singida Black Stars katika mchezo wa Nusu Fainali Jumanne, wakati Jumatatu itachezwa Nusu Fainali ya kwanza kati ya Azam FC na JKU.

Comments