WAZIRI wa Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu, Ridhiwani Kikwete akitoa taarifa ya ukamilifu na Utayari wa maandalizi ya kilele cha Sherehe za Mei Mosi zinazotaraji kufanyika tarehe 1 Mei, katika viwanja vya Bombadier, Manispaa ya Singida.
Taarifa hiyo ameitoa kwa Kassim_Majaliwa , Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania .
Akizungumza baada ya ukaguzi na kupokea taarifa, Waziri Mkuu wa JMT ameeleza kuridhishwa na maandalizi na kupongeza maandalizi yaliyofanyika ambapo ameeleza kuwa na viwango vikubwa sana kuliko kupata kutokea.
Pia ametumia nafasi hiyo kuwakaribisha wananchi na wafanyakazi wote kwenda kusherehekea mafanikio ya miaka minne ya Mh. Rais Samia Suluhu Hassan.




Comments