CCM KUANZA UJENZI WA JENGO LAO LA KISASA LA MAKAO MAKUU

CHAMA Cha Mapinduzi  (CCM) kinaanza kujenga  jengo la kisasa la Makao Makuu jijini Dodoma mkabala na Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete.


Jiwe la Msingi la ujenzi huo litawekwa na Mwenyekiti wa  CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano, Samia Suluhu Hassan Mei 28 mwaka huu.

Hayo yameelezwa na Katibu  wa Itikadi,Uenezi na Mafunzo CCM, CPA Amos Makalla, alipokuwa akuzungumza na vyombo vya habari jiji Dodoma Mei 24, 2025, kuhusu maandalizi ya Mkutano  Mkuu maalumu  wa chama hicho  unaotarajiwa kufanyika Mei 29-30 katika ukumbi wa Jakaya Kikwete. 

CPA Makalla amesema kuwa Jengo hilo litakuwa la kisasa ambalo litakuwa na huduma zote muhimu na litaendana na hadhi ya CCM ambayo kwa sasa inawanachama zaidi ya milioni 11.

“Tunajenga jengo la Makao Makuu karibu na  Jengo hili ( Jakaya  Kikwete) ambalo litakuwa na facilities zote CCM ni Chama kikubwa Tanzania pamoja na Afrika,tumeona umefika wakati wa kuwa na jengo lenye facilities zote kumbi za mkutano, parking kwa sababu  Chama hichi ni kimbilio la  wananchi,”amesema  Makalla.


Aidha, amesema kuwa maandalizi kwa ajili ya Mkutano Mkuu maalumu  wa Chama cha Mapinduzi (CCM) yamekamilika na  unatarajiwa kufanyika Mei 29-30 katika ukumbi wa Jakaya Kikwete na utahudhuriwa na wajumbe 2000 wa mkutano Mkuu kutoka mikoa yote nchini..

Katibu  wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo CCM Taifa, CPA Amos Makalla,akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano huo.



Makalla akikagua maandalizi katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete.


IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA
MSIMAMIZI MKUU
KAMANDA WA MATUKIO ONLINE TV
0754264203

 

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

UKWELI KUHUSU TENDO LA NDOA NA FAIDA ZAKE

HUYU NDIYE WANU HAFIDH, CHAMPIONI WA ELIMU

MAWAZIRI WALIOACHWA HAWA HAPA

๐Œ๐‰๐”๐„ ๐Š๐€๐‚๐‡๐„๐‘๐Ž ๐Œ๐™๐„๐๐€

HISTORIA YA MAREHEMU MC PILIPILI

VITU 10 WANAUME WANAVYOPENDA ZAIDI TOKA KWA MWANAMKE — SIYO SURA, SIYO MWILI ❤️

USIKUBALI KUWA LOFA KWA MWANAMKE...

NAPE AWAPA UKWELI VIJANA